Surua
ni mojawapo ya magonjwa ya kuambukiza ambao una kiwango cha juu cha maambukizi
pindi mtu apatapo vimelea vya ugonjwa huu. Pamoja na kuwepo chanjo ya ugonjwa
huu bado Surua ni miongoni mwa magonjwa yanayosababisha vifo vingi va watoto
walio chini ya umri wa miaka 5 katika baadhi ya maeneo duniani hasa kwa nchi
zinazoendelea.
Surua husababishwa na nini?
Surua
huenezwa na aina ya virusi jamii ya paramyxovirus katika mfumo wa njia ya hewa.
Kwa sababu hii basi virusi hawa huenezwa kwa njia ya upumuaji.Baada ya kuingia
ndani ya mfumo wa hewa virusi hushambulia seli za utando wa nje wa njia ya hewa (respiratory tract
epithelium) na kuingia katika mzunguko wa limfu na kufika kwenye tezi za karibu
na kusambaa mwilini.
Muonekano wa Mgonjwa
Dalili
za awali za Surua huanza kuonekana baada ya siku 8 baada ya kupata maambukizi.
Mgonjwa huwa na mafua mepesi, homa, kukohoa na macho kuwa makundu. Baada ya
siku 2-4 tangu kuanza kuonekana kwa dalili za awali.Ukimchunguza mdomo wa
mtoto, ndani ya shavu utaona vidonda vyeupe (koplik spot) kwenye utando
mwekundu wa ndani ya mdomo. Hii ni dalili tosha ya kudhibitisha uwepo wa Surua.
Lakini vilevile mgonjwa anaweza kuwa na vipele vidogo sana ambavyo huanzia
usoni au nyuma ya sikio na kushuka chini kabla ya kutapakaa mwili mzima.
Athari
za Surua
Surua
husababisha maambukizi njia ya masikio, mfumo wa hewa (nimonia), ubongo (encephalitis),
misuli ya moyo (myocarditis). Surua inaweza kusababisha utapiamulo, upungufu
wa chembe sahani kwenye damu(
thrombocytopenia)
Matibabu
Hakuna
tiba maalum kwa ajili ya Surua. Lengo kubwa la matibabu ya Surua ni kuhakikisha
mgonjwa anapata mapumziko, maji ya kutosha na dawa ya kutuliza homa kama
paracetamol.
Kinga ya Surua
Surua
huzuiwa kwa urahisi kwa njia ya chanjo. Watoto ambao hawajapata chanjo ya Surua
wapo katika hatari kubwa sana ya kupata Surua.
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa