Rubella ni ugonjwa unaosababishwa na virusi
vya Rubella na kuenezwa kwa njia ya hewa.
Mara nyingi huwapata watoto wadogo ingawa unaweza kumpata mtu wa
jinsia yoyote kwa mfano; mama mjamzito.
Dalili zake hufanana na dalili za surua kwa mfano vipele vidogo
vidogo, homa, macho kuwa mekundu, uchovu wa mwili, vidonda kooni, na uvimbe
kwenye matezi.
Ugonjwa huu ukimpata mama mjamzito unaweza kuleta madhara yafuatayo kwa mtoto
(Congenital rubella syndrome);
Ø Mtoto wa
jicho,
Ø Matatizo
ya moyo,
Ø Kutokusikia
vizuri,
Ø Mtindio wa
ubongo(mental retardation)
Ø Matatizo
ya ukuaji wa mwili (growth retardation).
Kinga ya
Rubella
Rubella
huzuiwa kwa njia ya chanjo Rubella.
Kampeni
ya mwaka huu tutatumia chanjo mchanganyiko ya Surua Rubella (MR) kwa ajili ya
kutoa ulinzi dhidi ya magonjwa yote mawili (Surua na Rubella)
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa