
Suarez pia alifungiwa mechi tisa za kimataifa.
Shirikisho la soka la Uruguay lilielezea adhabu ya Fifa kuwa ni "uamuzi uliopita kiasi" na hakukuwa na "ushahidi wa kutosha".
Suarez sasa anaweza kukata rufaa katika mahakama ya usuluhishi wa michezo.
Fifa pia ilimtoza Suarez faini ya Faranga za Uswisi 100,000.
Suarez aliomba radhi kwa alichokifanya.
Liverpool imekuwa ikishughulikia uhamisho wa mchezaji huyo kwenda Barcelona.
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa