Translate in your language
Friday, May 30, 2014
UTATA WA UMRI WAMALIZIKA
Uchunguzi wa chama cha soka la Italia FIGC umebaini kuwa kiungo wa Lazio Joseph Minala umri wake ni miaka 17 na sio miaka 42.
Tovuti mmoja ya Afrika mwezi Februari ilisema Minala ambaye ni mzaliwa na Cameroon, ana miaka 42 na sio 17.
Tuhuma hizo zilisababisha uchunguzi rasmi uliosababisha mchezaji huyo kuhojiwa.
"Uchunguzi haujaonesha haja yoyote ya kuchukua hatua za kinidhamu" imesema taarifa ya FIGC.
Minala alijiunga na klabu hiyo ya Rome mwaka jana na kucheza katika michuano ya Viareggio ya vijana mwezi Februari.
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa