Usafiri wa kwenda na kutoka Mafia umekuwa gumzo kisiwani, hii ni kutokana na ushahuri unaotolewa na taasisi inayosimamia usafiri wa nchi kavu na baharini SUMATRA kuzuia kusafiri wa boti za abiria katika kipindi wanachoamini si salama kusafiri kwa abiria baada ya kuwa na taarifa za hali ya hewa zisizoridhisha kwa vyombo hivyo kutembea majini, ukizingatia kuwa vyombo hivyo ni duni kwa kusafiri katika bahari kubwa, kwani ni vya zamani na hakuna huduma kamilifu za kiusalama pindi itapokuwa na dharura wakati wa safari zao.
hii ni moja maoni yaliyotolewa na mmoja wa mdau wa usafiri wa kwenda na kutoka mafia aliyoweka facebook na kuomba watu waweze kuchangaia :-
USAFIRI KISIWANI MAFIA,umekua na adha kubwa ,mara kwa mara boti zinazuiliwa kusafiri kwa sababu hali ya bahari kuwa mbaya na inafikia siku tatu boti haziruhusiwi kutoka wala kuingia,SUMATRA wanaamua bila kuwashirikisha wadau(manahodha) ambao naamini wanaujuzi na umakini wa hali ya juu,kama huyu anayeliangalia gari alilopakia kabla hajaanza safari,hadi kesho zitafika siku tatu hatutoki wala kuigia kisiwani ilhali bahari imetulia na ilichafuka siku moja tu,SUMATRA liangalieni tatizo hili kabla ya kutoa amri,tunateseka
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa