
Akizungumza na .... Mapema leo Meneja wa Tamasha hilo, Daniel Nyalusi alisema kuwa, toka ZIFF imeitisha upokeaji wa filamu kwa ajili ya Tamasha hilo la 16 la Nchi za Jahazi mnamo Septemba 2012 na kuweka mwisho wa kupokea Machi 31, 2013, hata hivyo kukawa na msukumo mdogo wa upokeaji wa filamu toka Tanzania, tofauti na nje ambapo mpaka sasa wameshapokea filamu zaidi ya 200 kwaajili ya uchaguzi wa jumla.

Pia Nyalusi alisema kuwa, katika tamasha hilo ambalo mwaka huu linatimiza msimu wa 16, limesheheni mambo mbalimbali na kuwataka wadau kulisubili kwa hamu.
Aidha, Nyalusi alieleza kuwa, kazi hizo za Swahili Movie/Bongo Movie competition, ndizo filam zitakazotoa filamu Bora ya Kitanzania, filamu Bora ya Afrika Mashariki na maeneo mengine (Categories).
Hata hivyo, Nyalusi alitumia wasaha huo kwa wasanii wote kutuma kazi zao kwenye tovuti ya ziff ilikutuma kazi zao, ama katika ofisi zao za ndani ya Ngome Kongwe Zanzibar.
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa