Translate in your language

Friday, June 15, 2012

KODI YA KUINGIZA MAGARI NCHINI YAPANDA


SERIKALI imepandisha kodi kwa asilimia 20 kwa magari yanayoagizwa kutoka nje ya nchi, yaliotengenezwa mwaka 2004 kurudi nyuma.

Akizungumza jana bungeni wakati akisoma Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka 2012/13,  Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk William Mgimwa  alisema magari ambayo yalitengezwa kwa miaka minane iliyopita na zaidi kodi imepanda kwa asilimia 20.

Alisema lengo la hatua hiyo ni kuboresha huduma ya kuagiza magari ili wananchi waache kununua magari kuukuu, lengo likiwa ni kuboresha na kulinda mazingira.

Kutokana na hatua hiyo ya Serikali matarajio ni kwamba bei za magari zitapanda.
Pia katika hotuba hiyo, Waziri huyo alisema  kwamba kodi kwa wasafiri wa ndege itaongezeka kwa abiria wanaotoka kwenda nje ya nchi hadi Dola40 za Kimarekeni badala ya Dola30.

Abiria watakaokuwa wakisafiri kwa ndege safari za ndani ambao awali walikuwa wanalipa kodi ya Sh5,000 sasa watalazimika kulipa Sh10,000.

Katika hatua nyingine, Dk Mgimwa ametangaza kodi maalumu kwa namba binafsi za magari, wa Sh5 milioni  kwa miaka mitatu.

Alisema lengo la kurekebisha sheria ya kodi ni kukusanya Sh6,360 milioni na kuboresha Pato la Taifa

No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)