Translate in your language

Tuesday, November 22, 2011

STORI 2,BURUDANI NA SOKA


 


Machozi  apagawisha Bilz, Sheta ..
 

MWANAMUZKI  nyota wa muziki wa  Bongo Fleva, nchini  Hussein Machozi usiku wa kuamkia Nov 21 aliweza kupagawisha mashabiki wapenda  burudani kwa nyimbo mbalimbali ikiwemo nyimbo yake mpya ya 'Asante' ambayo ilipagawisha mashabiki ndani ya ukumbi wa Kimataifa Club Billicanas uliopo katikati ya jijini la Dar  es Salaam.
Katika shoo, iliyoanza usiku wa manane, Machozi aliweza kukonga nyoyo kwa nyimbo zake kadhaa ikiwemo ya 'Ajiri yako', 'Mzimu', 'Za mwizi 40, 'kafia gheto' pamoja na kibao hicho kipya cha 'Asante', ndani  ya shoo hiyo , ambayo alipanda na madansa wake, waliweza  k upagawisho vilivyo na kufanya shangwe za mara kwa mara kutoka kwa mashabiki waliofurika ukumbini hapo.
Aidha, kwa mujibu wa Dj Ibra ndani ya ukumbi huo, wiki  hiyo, Msanii mwingine wa Bongo freva,  Nurdin Bilal 'Sheta' anatarajia kuzindua albam yake  ambapo atasindikizwa na wasanii nyota mbalimbali nani ya ukumbi huo.
Wasanii watakao msindikiza Sheta katika uzinduzi wake huo ni pamoja na Mwana FA 'Binamu' anayetamba na kibao cha 'Alahiti', Barnabas, Amini, Dully, Ay, na wasanii wengine wengi ili kunogesha zuzinduzi huo.
Kwa sasa Shata ambaye ni Rais wa Da stamina,  anatamba na vibao vya Unidai, sikudai aliiyoitengeneza kwa a Marcho Chalii na vibao vingne.
 
Mwisho


Sekondari ya Tirav wababe bonanza  la Tupambane Organization

SHULE ya Sekonari ya Tirav ya Jeti Lumo jijini Dar es Salaam, imefanikiwa kutwa  ubingwa  wa kombe la la Tupambane Organization  lililoshirikisha shule za Sekondari Kata ya Yombo Vituka.
Katika Bonanza  hilo, ambalo lilikutanisha timu za sekondari za  Lumo, Montefoty, Tirav na St.Moses, lililofanyika kwa siku mbili kwa lengo la kutoa elimu ya Ujana katika VVU na upimaji wa virusi, lilishuhudia mchezo mkali na wa aina yake wa fainali ya bonanza hilo lilifayika mwishoni mwa wiki kwa timu hiyo ya Tirav SS Fc  ikiinyuka Lumo SS Fc kwa bao 6-1 na kutawazwa kwa washindi wapya  na St.Moses SS Fc wakiibuka washindi wa tatu kwa kuwabwaga Monte foty SS Fc.
Awali  uhondo wa Bonanza hilo, ilishuhudia, Monte forty SS Fc  ambao waliua vibonde katika mshindano hayo, walikubali kichapo kichapo cha bao mbili bila dhidi ya Lumo SS Fc,  huku Tirav S.S FC wao  wakifanikiwa kuwabamiza  bao tatu  kwa moja,  St. Moses S.S Fc.
Mabingwa hao Tirav SS Fc, ilikua na wachezaji nyota mbalimbali akiwemo kipa wake mahiri aliyekua katika mafunzo maalum ya Aitrlrising star,Denis  Dionis 'Odo Nombo' ambaye alikua mwiba kwa kuokoa mashuti ya wapinzani wake,wengine ni Juma Kalufya  aliyekua akichezea Azam Fc, Under 17 kwa sasa Simba SC Un 17, pamoja na Abdul Lugume anaye chezea Villa Squad Fc, Un 17.
Mashindano ya kila mwaka,  washindi walipata zawadi mbalimbali ikiwemo vifaa vya michezo, ambapo Mwenyekiti wa Tupambane waliodaa hilo, Claudio Mnari alipongeza viwango vilivyoonyeshwa na watopto hao huku akitaka changamoto zaidi kwa mwakani kuongeza timu  ikiwemo kutokja nje ya kata hiyo.
"Mwakani tunatarajia kuongeza timu hili kuleta changamoto na pia wadau tunaomba kujitokeza ili kupiga tafu katika michezo" alisema Mnari.
Mwisho

No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)