Translate in your language

Friday, October 7, 2011

JUANI WATISHIA KUJITOA MRADI WA MAJI

 Mtendaji wa kijiji cha juani- Mafia akisoma agenda katika mkutano wa kijiji, agenda mojawapo ilikuwa ni kuchangia fedha za mradi wa maji toka Benki kuu ambapo wametakiwa kuchangia kiasi cha shilingi milioni nne ili waletewe huduma hiyo ya maji ya kisima katika kijiji iko ambacho ni kisiwa kiasili

(kila mwanakijiji anatakiwa kuchanga kiasi cha shilingi 1000/= tu kwa mwezi)
 Wageni katika mkutano huo kutoka Halmashauri, watatu toka kushoto ni Mhandizi wa maji, Afisa Tarafa na Mama Maendeleo ya jamii

 
 wanakijiji wakisikiliza kwa makini katika mkutano huo wa kijiji, wazee kwa kiasi kikubwa walikubali kuchangia mradi huo kwa manufaa ya kijiji, kwani maji ni mtambuka, yanahitajika katika huduma za afya lakini pia kuwavutia wafanyakazi kwenda na kufanya kazi eneo hilo kwani bila maji hakuna atakaekubali kwenda


Na vijana nao walikuwepo, kwa kiasi kikubwa hao ndio waliotishia kutochangia mradi wa maji na kutaka waendelee kuteseka kwa kufuata maji utende upande  mwingine wa kisiwa
Hii ndio aza wanayokupambana nayo watu wa kijiji cha juani kwa sasa kwa  kutumia vyombo vya bahari kama boti na jahazi kuja upande mwingine wa kisiwa kufuata maji

No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)