Translate in your language

Monday, May 9, 2011

Maige akamata mikoko ya magendo ikipelewa Zanzibar

Na Mwandishi Wetu


WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Bw. Ezekiel Maige amekamata shehena ya miti aina ya mikoko wilayani Mafia ikisafirishwa kimagendo kupelekwa Zanzibar.Hatua hiyo ya 
Waziri Maige ni dalili kuwa jitihada za serikali kupambana na uvunaji na usafirishaji haramu wa mazao ya misitu zimeanza kuzaa matunda.

Waziri Maige aliyekuwa katika doria baharini katika mikoa ya Lindi na Pwani akitumia boti maalumu ya ukaguzi alikamata jahazi lililosheheni mikoko 560 yenye thamani ya sh 4, 480,000 katika eneo la Bahari ya Hindi lililopo wilayani Mafia.

"Huyu hana kibali cha kumruhusu kuvuna mikoko, hana leseni ya kufanya biashara hii wala hati ya kusafirishia mazao ya misitu," alisema Arjason Mloge, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi anayesimamia matumizi ya mazao ya misitu katika Wizara ya Maliasili na Utalii ambaye aliambatana na Waziri Maige.

Kwa upande wake, Nahodha aliyekuwa akiongoza jahazi lililokamatwa na mikoko hiyo alisema amekuwa akifanya biashara hiyo kwa muda mrefu na mara zote amekuwa na nyaraka muhimu ila safari hii ndo hakuwa na vibali hivyo.

"Nimekuwa nikisafirisha mazao haya kwa muda mrefu na siku zote nimekuwa na vibali. Mwenye hii mizigo aliniambia nitangulie na mizigo na tutakutana huko akiwa navyo…sikujua kama natakiwa kuwa navyo nikiwa nasafiri," alisema Sirimu Ali Dai ambaye ni nahodha wa jahazi hilo lilokuwa likitoka Kilwa kuelekea Unguja.

Akizungumza baada ya kumkamata nahodha huyo, Waziri Maige alisema kuwa vitendo vya usafirishaji wa mikoko na mazao mengine ya misitu kinyume na sheria vimekuwa vikikua kwa kasi na kusema izara yake imejipanga kupambana navyo.

"Hali ya usafirishaji kiholela wa mikoko na mazao mengine ya misitu kupitia baharini imekuwa ni ya kutisha… tutahakikisha tunakabiliana na hali hii," alisema Waziri huyo baada ya kukamata mikoko hiyo inayokadiriwa kujaza malori mawili makubwa.

Waziri Maige alielekeza kuitwa kwa Afisa Misitu wa Wilaya ya Mafia, Bw Waziri Mkumbwa ambaye alifika na kukabidhiwa watuhumiwa, jahazi na mazao yaliyokamatwa na kuwafikisha polisi ili taratibu za kisheria zifuatwe.

No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)