Salam,
Tunapenda kutoa shukrani zetu za Dhati kwa watanzania wote waishio LONDON UK walioweza kufika jana jioni AFRICAN VILLAGE BAR & RESTAURANT kuchangia waathirika wa Gongo la Mboto Tanzania. Kwa mda wa masaa mawili
tumeweza kukusanya Jumla ya pesa taslim Pounds £600, pia tumekusanya Nguo nyingi kutoka kwa watu mbalimbali na vifaa vingine mbali mbali.
Ningependa kutoa shukrani za dhati kutoka URBAN PULSE,MISS JESTINA BLOG,AIL TV, LOCUS IMPEX SHIPPING CO, SHILLA FRISCH, NA Utawala wa AFRICAN VILLAGE BAR & RESTAURANT LONDON kwa kusaidia na kuwezesha kufanikiwa kwa zoezi la jana.
Mungu Ibariki Africa, Mungu Ibariki Tanzania
Asanteni
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa