Mpoto kuwasha moto "Shangwe Za
Muafrika"
Muafrika"
Mzalendo Pub Januari 13/kesho
MSANII nguli wa kughani mashahiri ya kuteka hisia za watu wengi nchini Mrisho Mpoto leo anatalajia kuwasha moto na Bendi yake ya 'Mjomba Band' ndani ya ukumbi wa Mzalendo Pub uliopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam .
Akiongea na waandishi wa habari blog Mpoto alisema kuwa atafanya mambo makubwa ndani ya ukumbi huo na hiyo itakuwa ni kila Alhamisi na itajulikana kama 'Shangwe Za Muafrika' ambapo nyimbo mbalimbali zitapigwa.
Mpoto alisema kuwa wamejiandaa vya kutosha kutoa burudani ndani ya ukumbi huo kila Alhamisi huku kukiwa na kitu cha pekee ambacho alichokipa jina la 'Hoja ya Mlevi'
"Nimejiandaa vya kutosha wadau wa burudani watafurahia na kukonga nyoyo zao, njooni kushuhudia shangwe za muafrika nikiwa na wasanii wakali wakiwemo walioshiriki Tusker Project Fame" alisema Mpoto.
Wasanii hao ni pamoja na Sabrina John, Ismail Kipira, Brian, Shaaban, Vasmo, Aneth Kushaba mshiriki wa 'Tusker Project Fame' na wengine wengi ambapo kwa pamoja watakuwa wakilishambulia jukwaa.
Aidha, Mpoto alisema katika uzinduzi huo wa leo utaudhuliwa na wadau mbalimbali wa burudani wakiwemo wanamuziki na wasanii wa nyota wa filamu sambamba na wafanyabiashara na mabalozi huku kiingilio kikiwa cha kawaida cha sh.5000.
Mbali na kukonga shoo, pia alisema kutakuwa na dakika 20 za mujadala na wadau watapata kutoa mada ama kuchangia mada maalufu kama 'Hoja ya mlevi'.
"Hoja ya mlevi, watu watapata kuchangia maswala yanayotugusa katika jamii, hivyo 'surprise' ya kesho (leo) tutajadili juu ya tatizo la Umeme na tukio la Arusha, ambapo kisha nitayatungia mashahiri na yataimba hapo hapo kila wiki na mengine" alisema Mpoto.
Mpoto anatamba na vibao mbalimbali kikiwemo cha 'Mjomba', 'Nikipata nauli', Adera na nyingine nyingi huku nyingine akiimba kwa kutumia mashahiri ya hapo kwa hapo
Pia alisema kuwa kila Alhamisi ndani ya ukumbi huo kutakuwa na wageni maalufu mbalimbali ambao wanamajina katika jamii sambamba na matukio zaidi ya burudani na kufahamiana.
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa