Translate in your language

Sunday, January 2, 2011

Wadau ZIFF waomba watanzania kununua filamu halisi




Na Andrew Chale, Zanzibar


MKURUGENZI wa Zanzibar International Film Festival (ZIFF), Profesa Martin Mhando amewataka Watanzania kuijitokeza na kununua kazi halisi ilikukuza soko na uchumi wan chi.


Prof.Mhando alisema hayo jana alipokuwa akiongea jana na waandishi wa habari ndani ya ukumbi wa ngome Kongwe, na kusema kuwa tayari wasanii wa Tanzania wamewewza kupiga hatua katika kutoa filamu mbalimbali ambazo nyingi kati ya zinamafundisho.


"Tumetoka mbali katika tasnia hii ya filamu kwa nchi yetu, hivyo kwa kuwa hii ni ajira rasmi, watanzania tujitokeze kununua nakala halisi ilikukuza soko letu ili filamu ziendeleze kukuza uchumi wan chi yetu" alisema Prof.Mhando.


Mbali na hilo, pia alishahuri Tanzania kuundwe Kamisheni ya filamu ambayo itasaidia kuletea nchi matunda mazuri huku Bodi ya filamu iliyoundwa ikiendelea kusimamia ushahuri na kamati mbalimbali za maadili.


Pia alisema kwa mwaka huu ZIFF imejipanga katika kuzipeleka filamu za watanzania nje ya nchi ili kushiriki katika matamasha makubwa ikiwemo tamasha la Afrika litakalofanyika nchini Bukinafaso mwezi Februari mwaka huu.


"Jumla ya filamu mbili zitakazoshinda leo (jana) kwenye tamasha hili dogo la ZIFF (Mini-Festival) zitaiwakilisha nchi kwenye tamasha la filam Afrika nchini Bukinafaso na bado tunaendelea na taratibu nyingine ili kuona filam zetu zinaonekana sehemu nyingi Duniani,"alisema Mhando.


Aidha, kwa upande wake Meneja Masoko wa Steps Entertainment Ignatus Kambarage aliwataka wananchi kujitokeza kununua nakala za filamu halisi ilikuweza kukuza vipato vya wasanii.


Anasema ukinunua nakala halisi unaongeza kipato cha serikali na hata kwa wasanii na wananchi kwa ujumla. Anasema baadhi ya wasanii waliokuwa ndani ya Steps Entertainment waliweza kuchangia watu wasiojiweza huko mkoani Mwanza hii ni matunda ya mauzo ya filamu halisi.


"Matunda ya filamu halisi yanasaidia kuitambulisha nchi na kuongeza matunda ya vyetu hapa nchini, hivyo tununue nakala halisi ilikuendeleza kazi zetu" alisema Kambarage.


Kampuni ya Steps ambayo inasambaza filamu mbalimbali huku filamu ya 'This is It' ya Steven Kanumba, 'My Briefcase' ya msanii Juma Kilowoko 'Sajuki' na 'Divorce' aliyocheza Masanii nyota Vincent Kigos 'Ray'.


Filamu hizo zote zimeingia katika kinyang'anyiro cha filamu nane kati ya hizo mbili zilitarajiwa kuchaguliwa kuingia kwenye Tamasha kubwa la filamu Afrika litakalofanyika nchini Bukinafaso mwezi Februari mwaka huu.




No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)