pichani baadhi ya wanakikosi cha 'action team'
Kikosi cha "Action Team' Mkoa wa Dar es Salaaam chatia fola sherehe za kuapishwa JK
Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania (Tanzania Red Cross Society) kupitia kikosi chake cha Maafa na Uokoaji cha 'Action Team' mkoa wa Dar es Salaam, leo kiliweza kutoa huduma ya kwanza kwa wananchi waliopoteza fahamu wakati wa sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete kwenye uwanja wa Uhuru jijini.
Kikosi hicho kilikuwa chini ya Kamanda Mkuu Dk.Suphian Juma sambamba na Feruz Mpili kamanda msaidizi waliweza kutoa huduma hiyo ya kwanza kwa wananchi mbalimbali hasa baada ya mizingia 21, kupigwa ambapo wanafunzi na akinama mbalimbali waliweza kupatwa na mishtuko hali iliyowalazimu kubebwa kwenye machela na kupatiwa huduma ya kwanza.
Wengi wa waliopoteza inadaiwa kuwa mbali na mizinga hiyo 21, ilipokuwa ikipigwa pia hali ya jua kali ilichangia kwa wananfuzno wengi kupata mshtuko na kupoteza fahamu huku kikosi hicho kikiangaika huku na huko kuokoa watu hao waliokuwa wameanguka chini na kuishiwa nguvu.
Akiongelea hilo , Kamanda mkuu, Dk. Suphian alisema kuwa licha ya kazi kuwa ngumu walihumudu na kutimiza lengo kwa kuwezqa kutoa huduma hiyo kwa ukamilifu huku kila mmoja aliweza kupata huduma stahili ilikuokoa na kuzuia matatizo na maafa zaidi.
"Tumeweza kubeba watu mbalimbali kwenye machela ilikuweza kupatiwa huduma zaidi, hivyo kwa waliopatwa na mshtuko walikuwa ni wengi sana na kikosi kwa umoja waliweza kufanya kazi hiyo ya kuwaondoa kila sehemu za majukwaa na kuwakimbiza katika mahema maalum ya kupatiwa matibabu" alisema Dk.Suphian.
Aidha, Dk. Suphian alisema kuwa tatizo hilo la kuanguka ambapo wengi wao walikuwa wanafunzi wadogo lilitokana na kukaa juani muda mrefu pia hali ya wao kuwa upande wa yanapopigiwa mizinga hiyo kilichangia kwa kiasi fulani.
Akielezea zaidi juu ya kikosi chake hicho cha 'Action Team' Mkoa wa Dar es Salaam , alisema kuwa kimejiandaa na kipo tayari kwa shughuli zote za dharura za maafa na uokoaji nchini kwani kipo tayari muda wowote huku shughuli zote zikiratibiwa chini ya Ofisi ya Mkoa na makao makuu ya Chama hicho cha Msalaba Mwekundu Tanzania .
Mwisho
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa