WATU sita wamekufa katika matukio tofauti Dar es Salaam, akiwemo mwanafunzi wa Shule ya Msingi Kibugumo, aliyekufa maji wakati wakiogelea na wenzake baada ya kumaliza mtihani wa darasa la saba.
Mwanafunzi huyo aliyetambuliwa kuwa ni Mahona Sukambi (14), mkazi wa Kigamboni,Dar es Salaam.
Mtoto huyo alikufa juzi saa nane mchana katika maeneo ya Kidete Beach wilayani Temeke.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Msime,mwanafunzi huyo alikuwa akiogelea na wanafunzi wenzake waliomaliza mtihani wa darasa la saba, lakini bahati mbaya maji yalimzidi nguvu, akazama, akafa.
Msime amesema,wananchi wa eneo hilo waliiopoa maiti ya mtoto huyo,imehifadhiwa katika Hospitali ya Temeke.
kwa maelezo zaidi bofya hapa
No comments:
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa