NFSC waomba msaada
UMOJA wa watoto waishio katika mazingira hatarishi na magumu mitaani ujulikanao kama New Hope Family Street Children-NFSC, umewaomba wadau kujitokeza na kuwasaidia vitu mbalimbali ikiwemo magodoro, vitanda na vyombo vya ndani.
Wakiongea na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa umoja huo, Omary Rajabu awaomba wananchi kujitokeza na kuwasaidia vitu hivyo kwa ajili ya kujiendeleza na maisha ya kawaida.
“Tunashukuru kwa kupata nyumba ya kupanga ambayo yumelipiwa kodi ya mwaka mmoja na wadau, hivyo tunaomba msaada wa haraka kwa kupata vitu hivyo ilikutusaidia katika matumizi ya nyumba hiyo” alisema Omary.
Umoja huo wa NFSC unajumlisha baadhi ya watoto na vijana mbalimbali waishio mitaani ambapo wamejiunga pamoja ilikuweza kutafuta huduma za kijamii ikiwemo kujiendeleza kielimu na kuishi maisha kama jamii nyingine ambapo wameweza kupata nyumba hiyo eneo la Ongindoni Kigmboni.
Kwa upande wake Katibu wa umoja huo, Hashimu Yusuph alitoa wito kwa mashirika na mataasisi watakaoguswa kujitokeza na kuwapatia msaada huo ambao utasaidia kupunguza matatizo yao .
“Magodoro,vitu vya ndani ama fedha tasrimu itasaidia kutimiza lengo letu la kujiendeleza tukiwa pamoja” alisema Hashimu.
Aidha, waliomba kwa atakayeguswa anaweza kuwasilina na Mhariri wa michezo wa gazeti hili ama kufika moja kwa moja zilizopo ofisi Mtaa wa Mkwepu Jengo la Billicanas.
No comments:
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa