"Wahoji kukatwa kwa Omary Kimbau, wataka ufafanuzi"
Na mwanablog wetu
KATIKA hali isiyo ya kawaida wananchi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mafia wapo njia panda ndani ya chama hicho kufuatia kutopatiwa ufumbuzi wa juu ya mgombea wao aliyeshinda kura za maoni na baadala yake Halimashahuri kuu ikampitisha mgombea mwingine.
Pichani;Omary Ayubu Kimbau (katikati)akisalimiana na Ridhiwan Kikwete(kulia) kushoto ni Idd Azan mgombea ubunge jimbo la Kinondoni.
Wakiongea kwa nyakati tofauti mapema jana kundi la wanachama wa CCM wilani Mafia, walipinga hatua ya kamati hiyo kuliondoa jina la Omary Kimbau aliyeshinda kwa kupata kura 1803 huku mpinzani wake ambaye alikua mbunge wa jimbo hilo Abdul Shaha akipata kura 1798.
Katika kile kilichoonekana kamati hiyo kucheza mchezo mchafu kwa Kimbau, wanachama hao walidai kuwa walitakiwa kupewa maelezo ya kina kwani wao walimchagua kwa moyo mmoja iliawatumikie jimboni hapo.
"Kwa kitendo hichi hamna sababu za kuwa na kura za maoni kwani mpaka sasa wameshindwa kuonyesha haki na thamani yetu wanaccm ndani ya chama kumpendekeza mtu tunayemtaka" alisema kiongozi mmoja wa chama hicho kutoka Kata ya Baleni amba akutaka jina
Mbali hilo, baadhi ya wanachama wa kutoka kata ya Kilindoni, Ndagoni,kigani,bweni na mburani wameamua kuweka mgomo baridi ilikushinikiza uongozi huo kutolea majibu ya kina na ya msingi juu ya kukata kwa jina hilo la Kimbau na kisha kulipachika jina Shaa la kuchukua maamuzi mazito ndani ya chama.
"Tunashazwa na ili lililofanywa na Kamati kuu kamwe halivumiliki kwa namna yoyote ile, tukimuuliza Kimbau anajibu tumuachie Mungu hii inatufanya tubaki njia panda tunaomba haki itendeke' alisema kada huyo aliye jitambulisha kama katibu wa Kata ya Ndagoni hakutaka jina
Hata hivyo alipotafutwa Kimbau kuongelea mstakabari wa mambo kufuatia hatua hiyo ya kamati kuliondoa jina lake, hakua tayari kuongelea swala
"Mimi sipo tayari kuongea na waandishi, hivyo juu ya swala langu kwa kina kamuulize Makamba ama Chiligati' Kimbau aliongea kwa upole na kukata simu.
Awali Kimbau alisisitiza kuwa hayupo tayari kuliongelea swala
Hali ya mambo ndani ya CCM tokea hatua za upigaji wa kura za maoni kumekua kukifukuta huku kila aliyeshindwa akimtuhumu mwenzake kua alicheza rafu, lakini kitendawili likamalizwa
Kati ya majina yaliyochujwa licha ya kushinda ni pamoja na Hussein Bashe jimbo la Nzega ambapo ilidaiwa kuwa si raia kwa jimbo la Iringa Mjini, Fredrick Mwakalebela alienguliwa kwa sababu ya kua na kesi ya rushwa ambapo wanachama walitoa lawama mbalimbali juu ya
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa