ZAM Foundation; Walimu wawe na taratibu za kutembezwa vijini
Na mwanablog wetu ,
Same-Moshi
SHIRIKA lisilo la Kiserikali la Zainabu Mgonja Community Foundation (NGO) limeitaka Serikali kuwa na taratibu za mara kwa mara za kuwapeleka walimu katika shule zilizopo vijijini na Kata ilikuweza kuzoea hali hiyo mapema na kulidhika kwa lolote litakalotokea , tofauti pindi mwalimu anapoamishiwa sehemu za vijini pasipo kuyajua mazingira ya sehemu husika.
Hayo yalisemwa jana Mkoani hapa na Mratibu wa ZAM Foundation, Salimu Mbaga wakati wa lipokuwa akikaribisha ugeni maalum (Volunteer) kutoka katika nchi ya Marekani na Uholanzi uliyofika Wilayani ambapo utafundisha masomo kadhaa pamoja na kubadilishana maalifa na wenyeji.
Salimu alisema kuwa walimu wengi wanakosa molali ya kufundisha pindi wanapohamishiwa kwenye shule za vijijini hii inatokana na walimu hao kutokuwa na taratibu ya kutembelea sehemu husika kabla uya kuhamishwa. "Mwalimu anahamishwa sehemu za kijini ambapo hakuwai kufika hata siku moja, hali hii inamfanya ajisikie mpweke na hata kukosa molalai ya kufundisha" alisema Salimu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa ZAM Foundation, Fatuma Kange aliomba wadau kujitokeza kusaidia taasisi zilizo vijijini ilikuweza kufanikisha ziara kama hii ilikuongeza chachu kwa jamii iliyopo mbali na mij hususani vijijini. "Mara zote timezoea kuona misaada mingi inatolewa mijini na kusahau jamii iliyopo vijini hii nisawa na kuwapunja haki zao za msingi" alisema Fatuma.
Nae mwalimu mkuu wa Shule ya Mwanya, Chanti Ngoka alishukuru kwa ujio wa wageni hao na kuhaidi kushirikiana nao muda wote wawapo shuleni hapo.
Wageni hao watafundisha katika shule ya Msingi Mwanya iliyopo katika Kata ya Makanya kijiji cha Kasapo kitongojii cha Mwanya Wilya ya Same Mkoa wa Kilimanjaro, watafundisha masomo ya Hisabati, Kiingereza pamoja na michezo , wagegeni hao ni Emilly kutoka Marekani, Lukas na Sjoird ambao wote kwa pamoja wanatoka nchi ya Uholanzi.
Pia wataunda klabu maalum kwa wanafunzi ilikujua mbinu za kuelewa masomo watakayofundishwa kipindi chote. 'Tumefurahia sana kufika hapa, watoto wateegee ujuzi na maalifa katika masomo yote tutakayofundisha" alisema Emilly.
Mwisho
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa