Tuesday, June 8, 2010

Mwanamuziki Oliver Ngoma afariki!!


Mwanamuziki wa Gabon Oliver Ngoma
Mwanamuziki mashuhuri kutoka Gabon Oliver Ngoma ameaga dunia.
Oliver aliyezaliwa Machi 23, 1959, alishamiri sana katika muziki ya Zouk na reggae, na alisifika sana pia kwa upigaji gitaa.
Aliingizwa katika fani ya muziki na baba yake ambaye pia alikuwa mwalimu wa ala mbali mbali za muziki.
Oliver alijiunga na bendi ya shule Capo Sound alipokuwa akisomea taaluma ya uhasibu.
Hata hivyo alionyesha uraibu zaidi wa muziki na akapewa ufadhili wa masomo ya uandishi na kupiga picha nchini Ufaransa.
Ngoma, aliyepewa jina la utani la Noli, alipata umaarufu zaidi kwa wimbo wake Bane, wa mwaka 1989 uliochezwa katika nchi zote za Afrika na ng'ambo.

No comments:

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa