WIZARA ya Habari,Utamaduni na michezo imeombwa kuangalia uwezekano wa kuongeza kiwango cha fedha kwenye idara ya utamaduni na michezo katika Halmashauri ya wilaya ya Manyoni ili iweze kufanikisha shughuli zake kama zilivyopangwa.
Ofisa utamaduni na michezo wa wilaya hiyo,Bona Masenge aliyasema hayon alipokuwa akizungumza kwenye semina ya siku mbili kwa walimu wa michezo wa wilaya ya Manyoni,Mkoani hapa.
Ofisa huyo mwenye dhamana ya michezo alisema ili kitengo hicho cha michezo kiweze kusimama chenyewe na kutekeleza yaliyopo kwenye ilani ya uchaguzi,ni wakati muafaka sasa kwa wizara hiyo kuangalia upya kwa kuongeza bajeti inayotengwa kwenye idara hiyo kila mwaka.
Kwa mujibu wa ofisa huyo hakuna ubishi kwamba bado kuna dhana potofu kwamba kitengo cha utamaduni na michezo ni kidogo,lakini dhana hiyo siyo kweli kutokana na shughuli za idara hiyo kuwa ni kubwa kuliko inavyotegemewa.
Akitoa mfano Masenge alisema katika bajeti ya wilaya hiyo ya mwaka wa fedha wa 2010/2011 idara ya utamaduni na michezo imetengewa zaidi ya shilingi milioni 18 kwa ajili ya shughuli zake,kiasi ambacho amesema ni kidogo ikilinganishwa na mikakati iliyojiwekea.
“Kwenye michezo peke yake kuna shilingi kama milioni sita hivi kwa sababu kitengo hiki kinaratibu pamoja na shughuli za mbio za mwenge kusema kweli hela hizi si nyingi sana hazitoshelezi shughuli za michezo kwa wilaya nzima kwani wilaya ni kubwa sana ”alisisitiza Masenge.
“Kuna shule za msingi 96 peke yake bado kuna shule za sekondari bado kuna wanamichezo wengine wa michezo ambao wote hao wana haki ya kuhudumiwa na idara ya utamaduni na michezo.”alisema
Naye mshiriki wa semina hiyo ya michezo,mwalimu Jonantande Thomasi wa shule ya msingi Makutopora alisema pamoja na mwaka jana kushiriki kwenye semina ya mchezo wa riadha na Valleyball na kuagizwa kwenda kutoa semina kwenye kata yao, hawakuweza kufanya hivyo kutokana na walimu wakuu kuwakwamisha kutekeleza mpango huo kwa kutowapatia shilingi elfu mbili tu kwa ajili ya chai ya washiriki wakati wa mafunzo hayo.
No comments:
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa