Translate in your language

Saturday, May 8, 2010



SIMBA SC YAKIPIGA NA EL HADOUD 


LEO HIIIIII


KIKOSI CHA SIMBA SC 2009/2010..LEO MEI 8 INASHUKA KATIKA DIMBA LA EL MAX 

 


Na Mwanablog wetu



WAWAKILISHI wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Simba, leo wanatarajia kukwaana na Haras El Hodoud ya Misri mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa El Max, mjini Alexandria nchini humo.

Simba iliwasilili jana mjini Alexandria ikitokea Cairo ilikopiga kambi ya maandalizi ya mechi hiyo ya marudiano; imetamba kuwaadhiri Waarabu hao kwao.

Kwa mujibu wa ofisa habari wa Simba, Cliford Ndimbo, wachezaji wote wako katika hali nzuri na wameahidi kutofanya makosa leo kwa kuhakikisha wanawafunga wapinzani wao na kusonga mbele.

Alisema licha ya kuwa mechi hiyo itakuwa na upinzani mkubwa, uhakika wa kuibuka na ushindi upo na hasa ukizingatia licha ya kujifua pia wamewajenga vema kisaikolojia wachezaji wao.

Katika mechi ya awali iliyopigwa jijini Dar es Salaam wiki mbili zilizopita, Simba ilishinda mabao 2-1, hivyo leo itakuwa ikipigana walau kuvuna sare ili kusonga mbele.

Simba inapaswa kupambana vilivyo hasa ikizingatia iko ugenini huku wapinzani wao wakiwa na bao la ugenini ambalo lilifungwa na  Ahmed Eid Abdemalek.

Wakali walioondoka na Simba ni Haruna Shamte, Salum Kanoni, Juma Jabu, Nico Nyagawa, Kelvin Yondan, Juma Nyosso, Mohamed Banka, Ramadhan Chombo, Musa Hassan 'Mgosi', Ulimboka Mwakingwe, David Naftal, Uhuru Seleman, Jerry Santo, Mohamed Kijuso, Emmanuel Okwi, Jabir Aziz na Joseph Owino.

                          

No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)