Na .....
CHAMA Cha Democratic Party (DP) kimetoa utaratibu wa kupata wagombea wa Urais,Ubunge,Udiwani na Viti maalum kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 huku fomu ya mgombea Urais ikipatikana kwa shilingi 50,000.
Katika taarifa kwa vyombo vya Habari iliyotolewa na mkurugenzi wa Uchaguzi, M.Mchunguzi ilisema kuwa fomu hizo za mgombea Urais anatakiwa kulipia kiasi cha shilingi 50,000 na anatakiwa kuwa na wadhamini 200 kutoka katika mikoa 16, Tanzania bara na Visiwani.
Ilieleza kuwa, fomu hizo zitatolewa kuanzia Juni 15 makao makuu ya chama hicho na kutakiwa kuirudisha Julai 15, ambapo kwa hatua hiyo ni pamoja na Zanzibar .
Mchunguzi alisema kwa upande wa Wagombea Ubunge na Uwakilishi watapata fomu hizo kupitia katika ofisi za majimbo huku kila mgombea anatakiwa kuwa na wadhamini 60, na fomu itakuwa shilingi 10,000 mbali na hilo, kwa wagombea wa Udiwani watachuklua katika ofisi za Kata huku wakitakiwa kuwa na orodha ya majina 40 na gharama ya fomu ikitolewa kwa shilingi 5,000.
Makundi mengine yatakayobahatika kupata fomu hizo bila malipo ni pamoja na wagombea wa viti maalum vya Ubunge/Uwakilishi na Udiwani ambao wao watatakiwa kuwa na wadhamini husika.
Aidha, katika taarifa hiyo ilieleza kuwa, makundi ya Wanawake,Vijana na Walemavu hawatagharamia fomu
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa