Translate in your language

Friday, April 23, 2010

RAIS KIKWETE KUONGOZA SIKU YA MALALIA DUNIANI!!

 

Na Mwanablog wetu



Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania  Jakaya Mrisho Kikwete  anatalajiwa kuwa mgenji rasmi siku ya maadhimisho ya ugonjwa Malaria yatakayofanyika Aprili 25 katika viwanja vya Mnazi Mmoja, ambapo kwa Tanzania  imepewa heshima ya pekee kuadhimisha kimataifa ikiongoza nchi zote Duniani.

 

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa leo jijini Dar es Salaam na  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Profesa David Mwakyusa (MB)  alisema hiyo ni fursa ya kipekee kwa Tanzania kuadhimisha siku hiyo ya Malaria Dunia, iliyokuwa na kauli mbiu ya "TUSHIRIKIANE KUTOKOMEZA MALARIA".

 

Mwakyusa alisema kuwa, kwa Tanzania kuadhimisha siku hiyo ni fahari ya pekee, huku macho yote ya wataalamu wa Mambo Duniani wakiwemo Wanasayansi,wanaharakati,wanasiasa,washiriki wa maendeleo na wanahabari na wapambanaji wa ugonjwa huo watayaelekeza siku hiyo ambayo ni ya Kihistoria kwa Watanzania.

 

"Hii ni kutokana na jitihada zetu za kupambana na ugonjwa huu wa Malaria, bila shaka zimeonekana, nijukumu letu sote sasa kuitunza heshima hii kwa kuongeza kasi katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria" alisem Mwakyusa.

 

Siku ya Malaria ufanyika kila terehe 25 ya kila mwezi wa Aprili, ambapo kihistoria siku ya Malaria ilianza kuadhimishwa  Aprili 25 mwaka 2000 baada wa nchi kukutana Abuja Nageria na kuamua kwa pamoja kuadhimisha kila ifikapo tarehe hiyo ilikuokoa madhara kwa jamii pamoja na kukumbuka jamii iliyokumbwa na ugonjwa huo ambapo ilijulikana kama "Siku ya Malaria Afrika".

 

Hata hivyo kuanzia mwaka 2008, ilibadilika na kuwa, siku ya Malaria Duniani, baada ya maafikiano ya mkutano wa Geneva Uswis katika mkutano wa 60 wa Afya Duniani mwaka 2007.

 

Mikakati ya kila nchi ni kupambana na ugonjwa huo kwa nguvu zote na kuhakikisha wanautokomeza ilikupunguza vifo kwa wananchi Duniani. Kwa Tanzania, Mwakyusa aliwataka watanzania kupigana kwa hali na mali ilikuhakikisha wanaushinda ugonjwa huo  ambao ni chanzo  kikibwa cha umasikini,Afya duniani na vifo vya wananchi wengi hususani watoto na walio na umri wa miaka mitano  na akina mama wajawazito.

 

Hivyo kwa kuona umuhimu wa kupambana na ugonjwa huo, Tanzania katika kuhakikisha inapiga hatua uimeweza kufanya mambo mbalimbali kwa wanachi dhidii ya ugonjwa huo, Mwakyusa aliytaja mambo hayo kuwa ni pamoja na : Tanzania kuanzisha kampeni maalum ya Zinduka iliyozinduliwa na Rais Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa mwanzirishi wa wa Umoja wa Viongozi wa Afrika wa kupambana na  Malaria, ALMA.

 

 Kushiriki katika chanzo ya kutokomeza Malaria,  Taasisi ya Afya ya IFAKARA imeweza kujulikana  ulimwenguni kutokana na tafiti zake za ugonjwa huo, visiwa vya Zanzibari vimeweza kukabiliana na ugonjwa huo mpaka kuushinda  na kuwa mfano wa kuigwa duniani kote,  kutoa huduma za Afya kwa bei nafuu, kugawa dawa za ugonjwa huo zikiwemo za ALU na mseto, kugawa vyandarua vya kudummu ambavyo vinadawa maalum ya kufukuza mbu na mengine mengi.

 

Mwakyusa alisema kuwa, mpaka sasa TANZANIA, tunakabiliwa  na tatizo hilo kwa asilimia kubwa, ambapo takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 93 ya watu wote wa Tanzania tupo katika hatari ya kuugua ugonjwa huo, huku ghala za kupunguza na tiba zinaigharimu  pato la Taifa takribani asilimia 3.4.

 

Huku idadi ya wagonjwa wanaokufa ni takribani 20,000 kila mwaka ambao kati yao alimia 80 ni watoto chini ya miaka mitano.

 


 

 


No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)