Translate in your language

Friday, April 23, 2010

 

MH. PINDA KUONGOZA MATEMBEZI YA KUCHANGIA ASASI YA MATITI APRIL 25 DAR

 

BI Angela kuzilwa kushoto na katikati ni Sophia Simba mwaka 2008

 

Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda anatalaji kuwa  mgeni rasmi katika siku ya matembezi ya Hisani ya kuchangia mfuko wa Asasi ya Saratani ya Matiti Tanzania.

 

Akizungumza na Mafia Blog, makao makuu ya taasisi hiyo yaliyopo Mwananyamala katika jingo la S&F  barabara ya Mwinyijuma, Komakoma, Mkurugenzi na mwanzilishi wa Taasisi hiyo Bi.Angela Kizilwa alisema kuwa matembezi hayo ya Hisani yaongozwa na Wiziri Mkuu,pamoja na mabalozi mbalimbali kwa kujumulisha wananchi.

 

"Mazoezi ya kuchangia mfuko wa Asasi tunatalajia kuyaanza  mapema siku ya Jumapili,25 Aprili ambapo yataongozwa na Mh.Pinda na kuanza kuanzia hospitali ya Ocean Road na kuzunguka sehemu mbalimbali kisha kumaliziki hapo hapo Ocean Road" alisema Bi, Kizilwa.

 

Bi.Kizilwa aliwaomba wadau mbalimbali kujitokeza katika matembezi hayo yaliyona lengo  mfuko huo kwa nia ya kutokomeza na kupunguza matatizo kwa wanawake wengi ambao wanakabiliwa nalo.

 

'Lengo zaidi ni kuona wadau mbnalimbali wakitupokea kwa kufanikisha dhima ya kupambana na tatizo ili ambalo si la akina mama waliokwisha patwa !! bali ni kwa ajili ya watanzania wote" alisema.

 

Kwa matembezi hayo yatakayofanywa siku hiyo yatakuwa ni ya pili kwa taasisi hiyo, ambapo mwaka juzi 2008 walifanya matembezi kama hayo yalitoa hamasa kubwa kwa akinamama kujitokeza kwenda kupima ama kuangalia afya zao na kukabiliwa na tatizo hilo kwenye Hospitali zilizojirani nao.

 

Katika matembezi hayo, ambayo yataongozwa na vikundi mbalimbali vikiwemo vya Ngoma, tarumbeta na bendi za shule, pia akimama ambao tayari wamegundulika na kufanyiwa operesheni ya ugonjwa huo, nao watakuwepo katika matembezi hayo.

 

Aliwataja wadhamini waliojitokeza kwa mwaka huu kuwa ni: IPP, Barclays, MSD,Twiga Cement,DHL na makamouni mengine mengi huku akiwataka wadau na makampuni mengine kuendelea kujitokeza kufanikisha misaada ambayo itaongeza ufanisi katika Asasi hiyo.


No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)