Wednesday, April 14, 2010

MAKALA MAALUM; VIFO VYA VIONGOZI WAKUU VILITABILIWA 

 

JANUARI 17, 2010 watu wote waliokuwemo katika kanisa la All Nations, na watazamaji wa kituo cha Televisheni cha  Emmanuel walishuhudia Nabii maarufu, TB Joshua akisoma orodha ya utabiri wake wa  mwaka kwa jumuiya za kimataifa na taifa.

 

Katika orodha hiyo ya utabiri ni ule ulioigusa Urusi na  nchi moja ya jirani, na kusisitiza watu wa Mungu kuliombea Taifa la Urusi na nchi hiyo jirani ambayo hakuitaja jina:

 

 

Jumapili, Machi 21, 2010  wakati akiendesha ibada Nabii TB Joshua alisema maneno yafuatayo:

 

"Nilikuwa katika maono na niliona parachuti ambayo ilikuwa imejaa watu – watu wengi walikuwa ndani ya parachuti. Lakini ilipoteza mwelekeo wakati ikiwa angani na parachuti ile ikawa inaangalia mahali pa kutua. Katika maono hayo nilikuwa nikiomba, "Mungu, … kama Mungu anaweza kunipa kibali cha kuitambua nchi hiyo, muda na wakati ambao tukio hilo litatokea,  ningefanya hivyo kuokoa roho. Lakini mimi ni mtumishi tu….

 

Siku hiyo hiyo ya Jumapili, ya Machi 21, 2010 wakati wa ibada hiyo hiyo, Nabii Joshua alifungua mambo mengi zaidi, wakati huu alielezea watu  aliowaona ndani ya parachuti ile.

 

" Nilisema lazima tuliombee taifa hilo, namaanisha hilo parachuti. Nilisema kuwa niliona Parachuti. Omba kwa ajili ya nchi hiyo kwa sababu naona watu waliomo ndani ya parachuti hiyo ni watu wazito, maofisa wa serikali.kuna kitu kitatokea angani. Nyoyo zao hazina hatia. Endeleeni kuwaombea.

 

Wiki iliyofuata, Machi 28, 2010 wakati wa misa iliyokuwa ikirushwa moja kwa moja kwenye televisheni, Nabii Joshua alielezea zaidi juu ya maono yake akisema kuwa  aliona bendera ikianguka chini.

 

"…ninaona bendera ikianguka chini. Ni nchi gani? Ninaona bendera– moja, mbili nyeupe….."

 

Jumamosi, Aprili 10, 2010, ghafla ikaja habari kuwa, Rais wa Poland, Lech Kaczynski, mke wake, Mkuu wa majeshi, Gavana wa benki kuu na maofisa wengine wa serikali ya nchi hiyo wakiwamo mawaziri na wabunge waliuawa baada ya ndege waliyokuwa wamepanda kuanguka nchini Urusi.

 

Habari za ajali hiyo, ziliishutua nchi ya Poland kama Waziri Mkuu wa nchi hiyo Donald Tusk alivyoilezea kwamba ni "tukio kubwa kutokea katika historia ya nchi hiyo ukiachana na vita vya kale".

 

Waziri Mkuu, aliitisha kikao cha dharura cha baraza la mawaziri baada ya kutokea ajali hiyo ambayo iligharimu maisha ya watu wengi.

 

Ni kweli Poland imepoteza watu wazito kama Nabii TB Joshua alivyotabiri, kwamba aliona maofisa wa serikali ndani ya parachuti.

 

Siku ya Jumamosi ndege iliyokuwa imebeba viongozi wakuu wa nchi na wanahistoria, akiwamo Rais wa nchi hiyo Lech Kaczynski, ilianguka karibu na uwanja wa ndege wa Smolensk, nchini Urusi, viongozi hao walikuwa  wanakwenda kuhudhuria kumbukumbu ya miaka 70 tangu kutokea  mauaji ya wafungwa wa vita wa Urusi na Poland waliouawa wakati wa utawala wa kisovieti..

 

Watu wote 96, waliokuwamo ndani ya ndege hiyo wengi wao wakiwa ni maofisa wa ngazi za juu katika siasa za Poland  walikufa papo hapo.

 

Miongoni mwa waliokufa katika ajali hiyo ni mke wa rais, Maria, Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje, Andrzej Kremer, Mkuu wa majeshi ya Poland, Franciszek Gagor, na Gavana wa Benki Kuu ya nchi hiyo, Slawomir Skrzypek. Abiria wengine waliokufa katika ajali hiyo ni wabunge na wanahistoria kadhaa.

 

Poland  imetangaza wiki ya maombolezo, Raia wengi bado hawaamini kile kilichotokea, hata kaimu rais,  Bronislaw Komorowski ana kazi ngumu ya kutambua nani watakuwa viongozi katika serikali ijayo ya Poland. Maswali mengi yamebaki juu ya ajali hiyo ya Aprili 10, kuhusu wale waliokufa, na wapi Poland inaelekea kutoka hapo ilipo.

 

Rais, Kaczynski na mke wameacha mtoto mmoja wa kike, Marta.  wajukuu wawili, mama wa rais huyo ambaye mgonjwa pamoja na pacha wake Jaroslaw ambaye alikwenda kuutambua mwili wake katika eneo la ajali.

 

Jaroslaw na Rais Kaczynski ni mapacha wanaofanana ambao utofauti wake unaweza kuutambua  kwa tabia na pete ya ndoa ambayo Kaczynski alikuwa nayo.

 

 Mapacha hao wawili mara nyingi walikuwa wakionekana pamoja kiasi kumepelekea kuibuka maneno kuwa Jaroslaw huenda akasimama kugombea nafasi ya urais aliyoiacha ndugu yake.

 

Wakati wakiwa watoto, mapacha hao walikuwa ni Mastaa wa filamu ya watoto  iliyokuwa ikijulikana kama "The Two Who Stole the Moon."

 

Mwaka 2005, jarida la Ireland la Times  liliwaandikia makala likieleza kuwa: Jarowslaw  alichukua masomo ya sayansi, wakati Lech yaye akichukua lugha. Na wote wawili wameshiriki katika siasa za nchi hiyo, lakini wote walipoteza umaarufu ndani ya jamii katika miaka ya hivi karibuni kutokana na kutetea uovu uliofanywa na maafisa wa zamani wa kikomunisti.

 

Hata hivyo, wachambuzi wanasema kuwa pamoja na hayo bado haizuiliki kwa Jaoroslaw, ambaye alijiuzulu Uwaziri Mkuu Novemba 2007, kuwa mgombea wa urais.

 

Wananchi ambao walihojiwa juu ya uwezekano huo, walionekana kuwa na masikitiko wakati huu wa msiba lakini baadhi yao walisema hawaoni kama pacha huyo anafaa kuwa mgombea.

 

Msemaji wa wizara ya katiba na sheria, alipuuzia akisema kuwa huu ni wakati wa maombolezo

 

Pamoja na hayo, maswali bado ni mengi, wengi wanajiuliza kwa nini Kapteni Arkadiusz Protasiuk pamoja na timu ya wafanyakazi wa ndege walipuuzia wito waliopewa kama kulikuwa na hali mbaya ya hewa hivyo wasingeweza kutua.

Je ni Rais yeye mwenyewe ndiye alipuuzia wito huo na kumuamuru Rubani aendelee kama alivyofanya mwaka 2008 wakati rubani alipokataa kutua katika eneo la Tbilisi, Georgia.

 

Kifaa kinachotumika kutunza kumbukumbu kinaonyesha kuwa, rubani alipokea taarifa za kumuonya. Na taarifa zinaeleza kuwa ndege ya Rais ilikwenda kwa ajili kuangaliwa kama ilikuwa iko sawa miezi minne tu iliyopita.

 

Serikali ya Poland: nini kinachotokea sasa

Rais wa mpito ana siku 14 tu za kupanga tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi tangu kifo cha Kacynski, na uchaguzi unatakiwa uwe ndani ya siku 60.

 

Hivyo basi, wananchi wa Poland watatakiwa kupiga kura kabla ya Julai 5 mwaka huu. Na kwa vyovyote vile chama cha kihafidhina cha Kaczynski huenda kikakabiliwa na upinzani mkali dhidi ya chama cha spika wa bunge Komorowski cha Liberal. Komorowski anakaimu nafasi ya urais kwa sasa.

 

Kuna wasiwasi mwingine ambao umejitokeza: kufuatia idadi kubwa ya viongozi waliofariki sanjari na rais.  Kwa mujibu wa sheria za Poland zinaeleza kuwa ni rais tu ndiye anayeweza kuteua nafasi za viongozi kama wale waliokufa kwenye ajali, ingawa tayari, kaimu rais Komorowski amekwishafanya uteuzi katika baadhi ya maeneo yaliyoachwa wazi.

 

Rais Kaczynski aliyezaliwa June 18, mwaka 1949 huko Warsaw alichaguliwa kuiongoza nchi hiyo mwaka 2005 baada ya kupata asilimia 54 ya kura zote zilizopigwa. Rais huyo alisisitiza umuhimu wa Poland kuimarisha uhusiano mzuri kati yake na Marekani.

 

Aidha, rais huyo aliuunga mkono mfumo wa kuwa na makombora ya kujilinda uliopendekezwa na rais wa zamani wa Marekani, George W. Bush.


No comments:

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa