ni baadhi ya magari yaliyokwama kati ya magari 50 yaliyokwama janakatika eneo tata la marendegu. Magari hayo yalikuwa yanatoka Mkoani Mtwara na Dar.
Barabara hiyo iunganishayo wakazi wa mikoa ya Lindi na Mtwara wanapata adha kubwa mno kwani ni kilo 60 za barabara hiyo bado haijakamilika hali inayowafanya hata kulala njiani.
MBUNGE SINANI; JENGENI HOJA ZA KIMAENDELEO.
Wananchi wa kijiji cha Mbae kilichopo katika Manispaa ya Mtwara wametakiwa kujenga hoja za kimaendeleo na kuachana na majungu ya chini chini dhidi ya viongozi wao.
Wito huo umetolewa leo na Mbunge wa jimbo la Mtwara Mjini Mohamed Sinani wakati wa ziara yake ya kutembelea vijiji mbalimbali vilivyopo katika jimbo lake.
Aidha Mhe Sinani aliwaambia wananchi kuachana na minong'ono na majungu ya kupika dhidi ya viongozi wao kwani kufanya hivyo kunarudisha maendeleo nyuma.
Hata hivyo alifafanua kuwa kipindi hichi ni kipindi cha kutuliza akili na kutafakari ni viongozi wa aina ipi wanatakiwa kuchaguliwa na si bora kiongozi .
"kipindi hichi ni kipindi cha kutafakari kwa makini viongozi tunaowataka....viongozi watakao tuletea maendeleo...Alisema.
Mbali na hivyo wanakijiji hao wa Mbae hawakusita kueleza kero zao na kumshutumu Mbunge huyo kwakutowatembelea mara kwa mara kusikiriza kero zao.
Walieleza , Mbunge wao hutembelea hapo kijijini mara chake hivyo hawapati muda wa kueleza kero zao zinazowakabili kijijini hapo.
"kiongozi wetu huwa hafiki mara kwa mara... ukiona anakuja ujue kipindi cha kampeni kimeanza...nasi tumejipanga kutowachagua viongozi wasiotujali...walisema
Akijibu malalamiko hayo ya kutowatembelea wananchi wake ,Mh Sinani alikanusha na kusema si kweli na kuwa hao wanaosema yeye hawatembelei wananchi wake ana hoja zake binafsi.
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa