Translate in your language

Sunday, April 25, 2010

MAADHIMISHO YA SIKU YA MALARIA - MAFIA

Mkuu wa Wilaya Mh. Manzie  Mangochie akiwa na kofia ya njano ndiye aliyekuwa Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo
wasanii wa kikundi cha MLONGO SANAA TROUPE kikifanya maigizo katika uhamasishaji wa kuwahi
mapema na kupima malaria katika kituo cha afya na matumizi ya vyandarua kujikinga na malaria
watu walihamasika na kufika na kuadhimisha siku hii ya malaria  hasa kina mama wakiwa na watoto wao
kikundi cha sanaa kikiwa katika maigizo na nyimbo
 Mganga Mkuu Dk. Said Salhina akisoma taarifa ya hali ya malaria kwa wilaya ya Mafia na mafanikio ya zoezi la kupambana na Malaria kwa wilaya
Mratibu wa CHAMAMA (changia maendeleo mafia) chama kisicho cha serikali Dr Naomi akisoma taarifa fupi ya chama hicho kilichoratibu maadhimisho haya chini ya Idara ya Afya

kikundi cha sanaa kikifanya mambo yake (MLONGO CULTURAL TROUPE)
Mratibu wa uhamasishaji CHAMAMA akimwonyesha moja ya kifaa cha uhamasishaji kwa Mkuu wa wilaya vitakavyotumiwa na maajenti wa kubadilisha tabia juu ya malaria katika wilaya
katika picha hizo hapo juu. Mh Mkuu wa Wilaya anaonekana akigawa baiskeli kwa maajenti wa kuhamasisha kubadili tabia
pia alikabidhi vyandarua vilivyo na viuatilifu kwa wamama walio na watoto wadogo walio na hati punguzo
picha ya mwisho Mkuu akimsisitiza mama kutumia chandarua iko hasa kwa mtoto husika ili kumkinga na malaria

No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)