Translate in your language

Sunday, March 28, 2010

WAFANYAKZI KIBASILA KUMUONA  LUKUVI KWA MAANDAMANO

 

WAFANYABIASHARA wa soko la Kibasila kesho Jumatatu...wanatarajia kufanya maandamano hadi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi, kwa lengo la kumfikishia malalamiko yao kuhusu kusimamishwa kwa uongozi wa soko hilo.

 

Akizungumza na mwanablog wetu hivi karibuni, mwenyekiti wa wafanyabiashara wa soko hilo, Edward Mwimazi, alisema uongozi wao ulisimamishwa tangu Machi 18 baada ya kamati ya maendeleo ya Kata ya Gerezani kuwakabidhi barua kwa madai kwamba uongozi wa soko hilo haujawahi kuitisha mkutano tangu ulipochaguliwa mwaka 2007.

 

Mwimazi alisema kabla ya uongozi wa kata kukutana na wananchi Machi, uongozi wa Kata uliwasilisha barua ya mkutano siku ya pili ambao ulikuwa na madhumuni ya kuzungumzia maendeleo mbalimbali ya soko hilo.

 

Mwimazi alisema anachokiona ni siasa zinazotendeka sokoni hapo kwa sababu Machi 18 katika mkutano huo waliohudhuria walikuwa ni viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Jeshi la Polisi na viongozi wa mitaa ambao wamejipa madaraka ya kuliongoza soko hilo.

 

Alisema mkutano huo ulitoa taarifa za utafiti wa mapato yaliyokuwa yakikusanywa, lakini kinachofanyika sasa wameanzisha mapato mengine mapya na kuyajumlisha pamoja ili kusaka visa ili uonekane uongozi haufai.

 

 Naye Ofisa Mtendaji wa Kata ya Gerezani, Fabian Nyange, alisema habari zilizotolewa na Mwimazi zinaupotoshaji kwa sababu uongozi wao tangu umeingia madarakani mwaka 2007 ulitakiwa ushughulikie katiba ya wanachama sokoni hapo, jambo ambalo bado haujalifanya!

 


No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)