MKE wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mama Salma Kikwete anatalajia kuwa mgeni rasmi katika siku ya kuwakumbuka akinamama waliopoteza maisha yao kutokana na uzazi mjini Mtwara Machi 15.
Akizungumza na katika kipindi maalum hivi karibuni, jijini Dar es Salaam katika kituo cha rredio ya shirika la Utangazi,TBC1, Mwanaharakati wa Utepe Mweupe, Daudos Tibaijuka alisema kuwa amefika wakati wa Serikali kuongeza nguvu kusaidia wanawake wajawazito mpaka wakati wa kujifungua kwao.
“Swala la vifo vya akinamama vinavyotokana pinmdi wanapojifungua, vinaweza kuhepukika, cha zaidi ni kuhakikisha Serikali inaongeza fungu maalum samba,ban a kuongeza vifaa kwa akinamama hao” alisema Tibaijuka.
Siku ya Utepe mweupe kuwakumbuka akinamama waliopoteza maisha kutokanana uzazi kitaifa ambapo inatarajiwa kufanyika kesho mkoani Mtwara, mgeni mwalikwa anatarajiwa kuwa mama Salma Kikwete , huku kauli mbiu ya Mwaka huu; ‘Bajeti ya Afyaya Mama na mtoto wakati wa kujifungua haijulikani’, Wekeza wekeza kwa ajili ya afya ya mama na mtoto ilikupunguza umasikini na kuboresha Uchumi’.
Vifo vinavyowakuta akinamama wakati wa kujifungua, alisema kuwa vingi vinatokana na akinamama wengi kupoteza damu nyingi wakati wa kujifungua pamoja na ugonjwa wa fistura ambao umekuwa ukiwakabiri wajawazito wengi wanaocheleweshewa kupatiwa huduma wakati wa kujifungua.
Asilimia 50, ya wanawake wanachangia nguvu kazi katika kilimo nchini pamoja na majukumu ya kuhudumia familia. Sherehe hizo ambazo imeandaliwa na Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama(White Ribbon Alliance for Safe Motherhood Tanzania-WRATZ) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
MWISHO
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa