Translate in your language

Sunday, March 28, 2010

EXIM BANK WATAKIWA KUJITUMA!!

 

MWENYEKITI wa Benki ya Exim, Yongesh Manek, amewaasa  mameneja wake kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza tija ya benki hiyo inayokua kwa kasi.

Manek alisema kufanya kazi kwa bidii kutaisaidia benki hiyo kukabiliana na ushindani miongoni mwa benki hapa nchini.

Akizungumza  katika mkutano wa mameneja wa benki hiyo nchini, uliofanyika mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam, Manek alisema hivi sasa Tanzania ina benki 37 hivyo kujituma miongoni mwa watumishi wake ndiko kutakakoboresha huduma za benki hiyo na hatimaye kukabiliana na ushindani.

Aliwaasa mameneja hao kufanyaka kazi kwa bidii na kuwakuza kitaaluma wafanyakazi walio chini yao, ili nao waongeze ujuzi katika kutoa huduma kwa wateja.

Menek ambaye alimkabidhi tuzo ya Meneja Bora wa Mwaka, Meneja wa Exim tawi la Mt. Meru Hamad Said, alisema tuzo hiyo ni changamoto kwa mameneja wengine kufanya kazi kwa bidii zaidi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Exim, Sabetha Mwambeja, alisema ukosefu wa miundombinu bora kama barabara ni kikwazo kikubwa cha benki nyingi kwenda vijijini.

Alisema baada ya kila mkoa kuwa na tawi la benki yake, watahakikisha kwamba huduma zake zinasambaa kwenye wilaya nyingi hapa nchini.

 


No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)