Exclusive Interview na Jokate Mwegelo. on March, 2010Blog yetu ilibahatika kufanya Interview na mlimbwende Jokate Mwegelo ambaye aliwahi kuwa Miss Vodacom Tanzania 2006 kulibeba taji lake vizuri mpaka alipomaliza muda wake,binti huyu amebarikiwa kuwa na vipaji vingi sana ni vipi hivyo fuatilia Interview hii kwa umakini zaidi upate kujua ni vipaji gani…. SWALI: Jokate Mwegelo ni nani? JOKATE:Jokate Mwegelo ni msichana ambitious, hardwoking, focused, the third born of the family of four kids, ni mwanafunzi vilevile anajishughulisha na mambo mbali mbali ya kielimu na wanamitindo and a lot more to come. SWALI: Je, unahisi ndoto ulizokuwa nazo utotoni zimetimia? JOKATE: Naweza kusema may be foundation ila ndoto zenyewe bado hazijatimia, nilipokuwa mtoto nilikuwa na ndoto ya kumaliza digrii bado haijatimia. Nina ndoto ya kuwa mtu mmoja ambaye anafanya maamuzi makubwa ya nchi hii bado haijatimia. Nina ndoto ya kuwa na my own thing going on bado hajatimia lakini naweza kusema so far the foundation has been laid down ambazo at least zinanisaidia kujenga sasa yale ambayo nadhani ningependa yatimie katika maisha yangu. SWALI : Nini kilikuvutia kwenye fani ya urembo? JOKATE: Kilichonivuta ni kuwakilisha nchi yangu, nilikuwa najiamini kwamba naweza kuwakilisha nchi yangu vizuri sana, na kuwa good ambassador katika masuala ya kijamii na kutetea masuala ya kijamii na ile whole experience ya kumeet new people at the tender age na kuwa exposed na fani yenyewe ilinivutia. SWALI: Je, wewe ni mwanamuziki? JOKATE: Mimi sio mwanamuziki, hapana….that happened I was just helping out a friend I thought the idea was nice so I was more than happy to be party of the project, a little project. Kwa sasa sina mpango wa kuendelea na hilo. SWALI: Role model wako ni nani? JOKATE: I have a lot of people who inspire me,… I can not identify a specific person but I think it goes on to any body who has breaking barriers. The thing ambayo inaweza kuku-insipire ni jinsi gani mtu ame-break that barrier na kufikia malengo yake. There are people like Oprah Winfrey, started from nothing but now she become the first black milionea, Hillary Clinton akagombea kuwa rais wa nchi yenye nguvu kuliko zote duniani, akina Anna Tibaijuka, you are talking about Angelique Kidjo musicians who are active in the entertainment but are also social consious umeelewa, wameweka jitihada na wanaona matunda ya jitihada zao. So they inspire me and I look up to them, even in Tanzania we have personalities ambao you can say wow! So sina mtu yule mmoja ambaye naweza nikasema nim-identify. SWALI: Unautumiaje muda wa ziada? JOKATE: Muda wangu wa ziada nakaa na familia yangu, najishughulisha na masuala ya kanisani, vijana vijana wenzangu, movies with my friends. SWALI: Unawezaje kufanya masomo huku ukijihusisha na urembo, filamu na muziki? JOKATE: Yaa…I dont know I have no answer for that, only God ananisaidia. SWALI: Ni kitu gani ambacho hatukijui kuhusu Jokate Mwegelo? JOKATE: I'm a deep thinker and I get lost in my thoughts as a refuge I resolve to writing, speaking and in the present act on my thoughts. I'm beyond passionate about my country's development and general welfare. I strongly believe in politics that if applied well definitely works and it's not all about blah blah but really affects peoples lives in the most equitable way and it's aims at being inclusive . SWALI: Je, unadhani vijana wa sasa wanatumia ujana wao vile inavyotakiwa? JOKATE: Aaaaa…..hapana I think bado…..sijui mimi nimekulia tofauti kidogo…..unajua ujana bwana ndio kipindi ambacho you are at you top kick to say…..unakuwa uko daring, unaelewa na unawaza vitu ambavyo ni out of this world, na una-push for them to happen kwa sababu watu wengi wanakuwa wanaamini hauko stable…lakini mimi naona kama hiyo ni opportunity ….unajua tunahitaji vijana wale wanabiashara zao, wanaingia labda kwenye siasa lakini sio zile za kupiga mdomo tu zile za kufanya maamuzi unajua…….I think bado kuna changamoto nyingi sana vijana lazima wazifanyie kazi ….wapunguze starehe….starehe zipo lakini wafanya na kazi. SWALI: Ungepata nafasi ya kutatua matatizo yanayoikabili jamii yako, ni tatizo gani ungelipa kipaumbele? JOKATE: Kuna tatizo kubwa la patriotism (Uzalendo)…unajua mimi ni mtanzania tena sio tu mtanzania bali mtanzania halisi kwa maana namjali mtanzania mwenzangu. Ukisha fikiria hivyo chochote kile utakachofanya ujue kinamhusu mtanzania mwenzako hivyo automatically utazuia yale mambo ambayo unajua yatakuwa mabaya kwa jamii. Hautasikia mambo ya mafisadi. But what am saying is that utaona watu wengi wanajituma kulitumikia taifa lao. Nakufanya maamuzi ambayo anaona nikifanya hili hapana hata kama rais hajui. Hilo ndio tatizo kumbwa ambapo watu watakuwa wakijali nchi yao, services zitakuwepo, watu watakuwa na muamko, hamasa ya kufanya vitu katika kujenga taifa. SWALI: Vipi kuhusu mipango yako ya baadae? JOKATE: Mipango yangu ya baadae nataka nijiendeleze zaidi kielimu, nataka nisome vizuri mambo ya mahusiano ya kimataifa, nataka nisome zaidi vitu vinavyohusiana na mambo ya international trade, national economy,International politics I want to do that hope full I work for government some how but again napenda kufanya public service, napenda kufanya my own thing, niwe na TV Program for example. I still have a lot to achieve. SWALI: Kwa sasa hivi unamalizia masomo uko mwaka wako wa mwisho chuo kikuu cha Dar es salaam hii inaonyesha umeweza kusoma bila matatizo,historia inaonyesha kuna warembo wengi,waliojiunga na chuo kikuu hawakuweza kumalizia elimu yao walihamia vyuo vingine nje ya nchi na humu ndani na sababu inadaiwa kwamba ni mizengwe ya wahadhiri wa chuo hicho kwa wasichana ambao wanakuwa ni maarufu, Je nini siri yako mpaka sasa umesoma bila matatizo? JOKATE: Siri ni bidii halafu ukiingia pale usijifany we staa bwana unaelewa? Umekwenda pale kusoma sio kufanya showtime……kule ni academics sio showbizz….watu wanataka wakuone umekwenda kule unachimba kwenye vitabu unaingia darasani. Naweza kusema attitude nilioingia nayo pale shule kwamba hii ni academical ground. Naamini kweli shule ni kichocheo cha mabadiliko ya maendeleo. Mimi najua uwezo wangu, shule ni kitu nilichokiwekea kipaumbele katika maisha yangu, halafu nikiwa shuleni nafanya vizuri sina historia ya kufanya vibaya kwa hiyo nikasema kwa nini nikija hapa chuo kikuu nishindwe. SWALI: Unadhani kuwa wewe ni tofauti na warembo wengine hapa nchini?na kwa nini unajiona wewe uko tofauti na warembo wengine? JOKATE: Obvious kila binadamu yuko tofauti ana vipawa vya tofauti na malengo yake tofauti. Siwezi kusema niko tofauti na warembo wengine lakini kama binadamu nimezaliwa tofauti na ninafikiria tofauti, nina muongozo tofauti na nina backgroung tofauti, mazingira niliyokulia ni tofauti na wengine ambayo pengine kwa namna moja au nyingine yameathiri jinsi ninavyofikiria na jinsi ninavyo-react to situations. So definitely am different. SWALI: Tunaelekea katika kipindi cha uchaguzi,Ukipata nafasi ya kuongea na Mbunge wa Singida mjini Mh.Mohammed Dewji ungempa ushauri gani au ungemwambia nini? JOKATE: Kwanza napenda kumpongeza unajua yeye anabiashara yake na anavitu ambavyo vinaendelea lakini ameona ajitoe katika kuamua kutoa maamuzi yanayowaathiri watu wake wa jimbo la Singida kwa hilo tu nampongeza na natoa chachu na changamoto kwa vijana wengine kuwa daring na kuweza ku-expand katika kuitumikia jamii. I think cha muhimu anipeleke Singida niweze kuona anavyofanya vitu vyake…..haha!!…napata good feed back anafanya vitu vizuri Singida….I think cha kutilia tu mkazo ni elimu, mimi kwangu elimu is the biggest thing. Watu wapate elimu sahihi isiyo na shida, vijana wapewe elimu na wapewe fursa waweze kujitambua zaidi na kujiendeleza. Unajua vijana sasa hivi sisi ndio tutakuwa marais, tutakuwa mawaziri so we have tu be empowered and empower our selves. Lazima tujidhatiti ili hata tukiwa viongozi wa baadae tunaongoza nchi vizuri. Sio unakuwa kama pilot halafu hujui geography. Kwa niaba ya MO BLOG tunapenda kumshukuru Jokate kwa kukubali kufanya nasi Interview na tunamtakia kila la kheri katika masomo yake na mwenyezi mungu amjaalie kheri aweze kutimiza ndoto zake maishani mwake. Hii na kwa mengine mengi, unaweza kutembelea ;Mtandao wa /www.mohammeddewji.com/blog..........kupata zaid |
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa