Translate in your language

Thursday, March 18, 2010

Dondoo soka za soka Bongo

 
‘Mo’ kuwapeleka Soka,Samata Simba kwa mkopo
 
Dondoo za Soka nchini, hivi karibuni iliweza  kupata taarifa kutoka vyanzao mbalimbali vya kuaminika nchini, viliifikia dondoo za Soka la Bongo kuwa, mmiliki wa klabu ya African Lyon, Mohammed Dewji, kuridhia wachezaji nguli na nyota wa timu hiyo pamoja na timu ya Taifa, MSHAMBULIAJI Yusuph Soka na Mbwana Samata kuichezea klabu ya Simba ‘Wekundu wa Msimbazi.
Taarifa hizo zilidai kuwa, wachezaji hao wataichezea klabu hiyo kwa mkopo kuanzia msimu ujao. AKwa hali hiyo mashabiki wa Simba ‘Fansi wa Simba’ walisema kuwa kwa hilo itaendelea kuipa jeuri Simba kuendelea kutetea Ubingwa wa  Ligi kuu msimu mqwingine “ Kwa hili  Simba imepiga bao na kuipa jeuri zaidi ya kuendelea kuvuna mataji ndani na nje ya nchi’ vilisema vyanzo vya Habari.
Mwisho
 
Papic, Twalibu wapigiwa debe Stars
 
Kufuatia kumalizika kwa mkataba wa Kocha wa Kibrazili, anayekionoa kikosi cha Taaifa Stars, Maxio Maximo, huku Shirikisho la Soka likitoa vigezo kadhaa vya kocha aliyena uwezo kujitokeza kuomba. Tayari kocha wa Yanga,  Kostadin Papic ambaye ndiye kocha wa kwanza kutuma maombi yake ya kukinoa kikosi cha Stars, huku Twalibu anayejiusisha na ufundishaji wa Soka Umangani akituma maombi yake, mdau wa Soka wa klabu maarufu nchini ametoa maoni yake na kutaka makocha hao wapewe kipaumbele.
Vyanzo hivyo kutoka katika mtandao mmoja maarufu kwa mashabiki wa klabu Kongwe hapa nchini, ulipokuwa ukifanya maojiano na mdau huyo, alinukuliwa kuwa; alisema kutokana na uwezo wa kufundisha kati ya makocha wote wanaogombea mikoba ya kumrithi Maximo , Papic ndiye anayestahili kuchukua mikoba hiyo kutokana na ukweli halisi kuwa ameweza kuibadilisha Yanga katika kipindi kifupi alichoifundisha.
Mbali na hayo pia kocha huyo ana uzoefu mkubwa na soka la Afrika hivyo akipewa stars huenda ikawa moto wa kuotea mbali.huku akimp[endekeza kocha msaidizi kwa anayefaa ni Twalibu. Ambapo alisema kuwa maoni yake hayo yasitafsiriwe vibaya kwani yeye ameongea kama watanzania wengine wanaotola maoni yao katika soka la Bongo.
Stockler  aipa shavu Simba kwa Ubingwa
 
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya vijana mbrazili Stockler amekiri kuwa simba ilistahili kuchukua ubingwa wa ligi kuu kutokana na maandalizi mazuri kuanzia ligi ilpoanza kwa kushinda michezo yote ya duru la kwanza .Simba hadi kuchukua ubingwa imeshinda mechi 18 ktk michezo iliyocheza na kutoka droo michezo miwili.
Sockler amesema kwa sasa soka la Tanzania limekuwa na limekuwa la kuburudisha zaidi kiujumla hivyo ni mafanikio na wachezaji waendelee kujituma zaidi kwani miaka ya karibuni Tanzania itaku kama nchi kubwa zilizo endelea kisoka.
Mwisho
Yanga yaitupa nje Moro Utd,Ligi kuu Bara
Kwa hali machi  iliyopigwa kati ya Yanga na Moro, huku Yanga ikichomoza kwa magoli 3-0, imeifanya klabu hiyo ya Moro kuyaaga mashindano hayo ya Ligi Kuu BARA.
Katika mchezo huo, Yanga ambayo tokea kuanza hatua ya pili ya ligi hiyo imekuwa ikicheza kwa kasi na kuvuna ushindi wa kishindo, huku mfungaji wake mahiri , Ngassa katika mchezo huo alikuwa tishio akipachika magoli mawili likiwemo la dakika 5 ya mchezo na dakika 14, ya mxchezo. Kwa kupachika magoli hayo, ameweza kufikisha goli 14 sambamba na mfungaji wa Simba Mussa Hassan Mgosi mwenye magoli 14.
Katika mchezo huo, goli la 3 kwa Yanga lilifumngwa na Ambani .ambaye pia ana mabao 14 kaatika kuwania mfungaji bora.kwa  ushindi huo yanga inaendelea kushika nafasi ya pili ikiwa na pointi 48.na Moro united kwa kichapo hicho imeshuka rasmi daraja ,hivyo kuzisubiri timu mbili amabazo itaungana nazo kati ya Manyema , Maji maji au Prison.
………………………………………………….
Usiyo yajua Soka kutoka fansi wa soka la Bongo
 
 
Hiii!! Imetokea mtaa wa Jangwani na Twiga
Kuna tetesi kuwa, klabu kongwe nchini za Simba na Yanga, ‘wanazi’ yaani mashabiki na wapenzi damu ndiyo wanaongoza kwa majungu ambayo kwa kiasi kikubwa ndiyo yanayopelekea hata kufukuzwa kwa baadhi ya wachezajin na hata viongozi.
“Pale Jangwani na Twiga, utakuta wazee kwa vijana kuanzia asubuhi mpaka usiku wamekaa wakinywa kaawa huku wakisoma magazeti kuanzia erufi ya kwanza hadi ya mwisho’ ukipita mchezaji au kiongozi wanaanza kujadili jambo flani’ alisema mwanasoka nyota wa Bongo ambaye sasa ni mfanyabiashara mkubwa wa magari aliyewai kuchezea Simba na Yanga. (jina kampuni).
Hata hivyo uchunguazi wa Tafakari kujua ukweli, uliweza kuwakuta wazee hao mtaa wa Twiga na Jangwani Maskani kwa Yanga African, huku ikipiga mbili tatu stori na wazee hao, ghafla mzee mmoja ‘akaropoka’ yule ajui uongozi wowote, kutwa kupiga domo….Mahakama hata siku mmoja ahatujawai kusikia anasikiliza ama kusimamaia kesi….Aaah?? acha wewe tusaidie 2500, ya kahawa,, alisikika mzee huyo.
Hata hivyo baada ya kuondoka yule mzee alisema unaona kama asingetoa tungemmshambulia na hata kumuwekea zengwe sisi ndiyo timu bwana

No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)