Na Andrew Chale
MWANAHARAKATI wa kutetea Haki za Watoto nchini na Mwenyekiti wa Chipuziki(CCM) Wilaya ya Kinondoni, Nimka Lameck (10) mbioni kutembelea watoto mbalimbali wakiwemo wanaonyanyaswa katika jamii pamoja na walio katika mazingira magumu.
Akizungumza na Tanzania Daima jana, msemaji wake, ambaye ni kiongozi wa UVCCM Kata ya Makumbosho, Hashimu Athumani alisema kuwa zoezi la kuwatembelea watoto mbalimbali hasa walio katika manyanyaso na wale waliokosa fursa muhimu za kijamii, na kukusanya kero zao.
“Katika kufikia malengo kama mwanaharakati na kiongozo wa watoto, Nimka anatarajia kuzunguka katika Kata 27 za Manispaa ya kinondoni kwa lengo hilo pamoja na kujenga mahusiano mazuri na watoto walioko mitaani ambao wengi wao wamekata tamaa” alisema Hashimu.
Kwa upande wake Nimka, alisema kuwa mbali na matarajio yake ya kutembelea Kata hizo 27, lengo ni kuhakikisha anawafikia watoto wote nchini na kupata kujua matatizo yao . “Siku zote watoto wengi wanakosa fursa ya kupata kutetewa na watoto wenzao richa ya kuwepo watoto walio na uwezo huo, hivyo na hakika kwa kuwatembelea kutahamsha hali za kikatili na manyanyaso mbele za jamii kupungua” alisema Nimka.
Mbali na kuwatembelea watoto hao, pia atatoa ujumbe mbalimbali kwa jamii pamoja na kutoa vifaa mbalimbali vya shule na mavazi kwa watoto wasio jiweza.
Mikakati ya kutembelea Kata hizo, zinatarajiwa kufanyika kuanzia Machi 6 hadi Aprili 3 mwaka huu, “Harakati hizi atazifanya kila siku za Jumamosi pamoja na Jumapili pekee, huku akitembelea baadhi ya vituo vya kulelea watoto yatima, mashule na walio mitaani” alisema.
Hata hivyo waliomba viongozi wa mashirika ya kiserikali na yasiyo ya Serikali kujitokeza kusaidia zoezi hilo ilikutimiza lengo la kuwasaidia watoto wa Tanzania .
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa