Sherehe za Maulid mwaka huu kitaifa zitafanyika mjini Mtwara.
Taarifa zilizopatikana kutoka Ofisi ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania zinasema kuwa, maadhimisho hayo ya Maulid yatafanyika usiku wa Ijumaa tarehe 26 Februari, 2010 kuamkia Jumamosi 27 Februari, 2010. Kufuatia maadhimisho hayo, siku ya tarehe 27 Februari 2010 itakuwa ni siku ya mapumziko kote nchini sawa na mwezi 12 Mfungo Sita. Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) linawatakia mapumziko mema Watanzania wote.
chanzo:MICHUZI JR
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa