Translate in your language

Sunday, February 7, 2010

Kikwete kuzindua Gati la Mafia

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi wa uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa  Gati kubwa na la kisasa kwenye Kisiwa cha Mafia.
 
Akiongea na Tanzania Daima  ofisini kwake jana, Mkuu wa Wilaya ya Mafia Manzie Mangochie alisema kuwa Rais anatarajiwa kuweka jiwe la msingi mwezi Machi mwaka huu na kuashiria maendeleo ya Gati hilo .
 
“Mpaka sasa mchakato dhidi ya ujenzi huo unaendelea vizuri na mpango wa kuakikisha Gati linajengwa ambao Rais aiuahidi huko nyuma,  umeananza kuzaa matunda na mwezi Machi anatarajiwa kuweka jiwe hilo la Msingi ilikuongeza msukumo” alisema Mangochie.
 
Mangochie aliwatoa hofu wakazi wa Mafia, ambapo aliwataka wawe na imani na Serikali yao pamoja na viongozi waliowachagua kuwa kero zao wanazifanyia kazi na Serikali kuzitolea ufafanuzi kadiri ya uwezo wake.
 
“Umeona mitambo kule baharini, ikiendelea na ujenzi hivyo si mambo mengine wananchi wayaone kwa macho, wakandsarasi wanayashughulikia kitaalamu nje ya hapo na baada ya kukamilika wanakuja kumalizia sehemu husika” alisisitza Mangochie.
 
Aliendelea kusema kuwa, ujenzi wa Gati hiyo ambao ujenzi wake unatarajiwa kuchukua miezi 12 hadi kumalizika kwake, unatarajiwa kuwa mkombozi kwa wananchi wengi wa  Kisiwa hicho ambao muda mrefu wanapata hadha ya usafiri.
 
“Ninahakika pindi ujenzi utakapokamilika utakuwa faraja kwa wakazi wengi wa Mafia na kupanua wigo wa kibiashara na vyanzo vya mapato kuongezeka” alisema Mangochie.
 
Pia alida kuwa, mbali na kutegemea usafiri wa anga, huku wakazi wengi wakishindwa kujikimu kulipia nauli ya ndge, kutokana na kipato chao duni, huku wakitumia usafari wa boti ambazo usalama wake ni mdogo, inafanya hata kusababisha upungufu mkubwa wa watumishi wa Serikali kutofika katika Kisiwa hicho.
 
“Halimashauri inarudi nyuma katika maendeleo, hivyo pindi Gati hiyo itakapo kamilika hitakuwa chachu ya kuvutia wafanyakazi na shuguli za kibiashara, hiki si kilio cha wakazi wa  Mafia peke yao , hata Serikali yenyewe inapata tatizo kubwa kila mwaka” alimalizia Mangochie.
 
Ukamilikaji wa Gati hiyo, kisiwa hicho kitaweza kuingiza meli mbalimbali zikiwemo aza kibiashara pamoja na zile za usafirishaji wa abiria ambazo zinakwenda kasi kwa kufanya usafiri wa haraka kutoka Dar es Salaam hadi Mafia, Zanzibar – Mafia.
 
toka chanzo muhimu cha habari  

No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)