Na mtandao
MJUE kwa undani mwanasoka nyota wa klabu ya Chelsea na nahodha wa timu ya Taifa ya Uingereza aliyekumbwa na jinamizi la kufanya ufuska nje ya ndoa yake.
picha ya John Terry
Kati ya mambo yaliyomkuta John Terry (29) yanaendana sambamba kwa kiasi kama yale yaliyomkuta mwanamichezo nyota wa mchezo wa gofu duniani Tiger Woods, hata hivyo baada ya Woods kushtukia kuwa vyombo vya Habari ndivyo vilivyochochea kashfa yake kuwa kubwa, aliamua kuvichunia na kupunguza makali.
Vannesa naye pia amewekwa katika kitabu cha Terry
lakini kwa upande wake Terry yeye mbali na kushauriwa kuacha kuzungumzia swala lake hilo na vyombo vya habari, alipuuzia na kupelekea Kocha wake wa timu ya Taifa ya Uingereza Fabio Capello kuamua kumvua unahodha.
Hata hivyo mbali na Capello kuamua uamuzi huo waq kumsimamisha unahodha ambao umekuja kushikiliwa na mlinzi wa timu ya Mashetani wekundi Manchester United, Rio Fedinand, vyombo vya Habari vilisha muukumu Terry kwa swala lake hilo .
Husiyoyajua ya John Terry
Majina yake kamili ni John George Terry, alizaliwa mnamo Desemba 7, 1980 katika jijini la London , Uingereza.
Terry ambaye ni mchezaji wa nyuma kati, alianza kuichezea klabu ya Chelsea ya Uingereza tokea akiwa na umri mdogo ambapo alikuwa akichezea timu ya watoto.
Alipoanzia kipaji chake;
Terry alipokuwa mdogo katika soka, aliweza kuichezea timu ya West Ham ya Vijana wadogo 1995 hadi 1998, na kisha kujiunga na Chelsea mwaka huo.
Alipokuwa kijana wa makamo;
Mwaka 1998 aliweza kuichezea klabu ya Chelsea , Mwaka 2000 alienda kwa mkopo katika timu ya Nottingham Forest
Mwaka 2000 hadi 2002 aliweza kuichezea timu ya Tifa ya Uingereza (U21).
Mafanikio zaidi;
Terry ambaye ni mzaliwa wa jiji la Londoni, aliwweza kuja kuwa Nahodha wa klabu ya Chelsea baada ya kuwika vilivyo hali ambayo kiwango chake kilionekana tishio katika ligi hiyo ya Uingereza (Premier League). Alaiweza kushika unahodha wa timu ya Taifa mwezi Agosti 2008 na kushikilia hadi mwezi Februari 2010 kutokana na kashfa yake hiyo ya kutembea nje ya ndoa.
Terry aliweza kuwika katika soka na kusababisha kuchaguliwa kuwa mlinzi bora kwa upande wa ligi ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA Champions League) katika kipindi cha mwaka 2005 na 2008.
Pia mwaka 2005, alichaguliwa kuwa mwanasoka bora wa mwaka na FA, mbali na kuchaguliwa huko, Terry aliweza kubaatika kuingizwa katika kikosi maalum cha FIFA (all-star),kwa kuchaguliwa kwake huko, kulifanya kuwa mchezaji pekee anayeichezea ligi ya Uingereza kuunda timu hiyo.
Mwaka 2007, Terry nyota yake ilizidi kung’ara baada ya kuchaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa nahodha wa timu hiyo,hii ni baada ya kuinyuka goli moja timu ya Manchester United, zilipokutana katika kombe la ligi ya (FA CUP) ndani ya uwanja wa Wembley.
Pia aliweza kuipatia goli timu yake ya Taifa goli moja dhidi ya vinara wa soka duniani Brazil na kufanya matokeo kuwa 1-1.
Hata hivyo, e 2007-08, katika misimu hiyo Terry na timu yake ya Chelsea aliwza kukosa makombe matatu ikiwemo mkushindwa katika kombe la ligi kwakati wa fainali dhdi ya Tottenham Hotspur.
Na katika ligi ya klabu bingwa, wakati wa fainali dhidi ya Manchester United, Terry aliweza kukosa mkwaju wa penati ambapo aliupiga na kupaa nje.
Wadhamini wa Terry
Terry aliweza kujipatia sifa mbalimbali katikia taalum yake hiyo katika soka na kuweza kujizolea wadhamni ikiwemo kampuni ya Umbro ambayo ilikuwa ikimdhamni mchezaji Michael Owen.
Mbali na kampuni hiyo, aliweza kuingia mkata na kampuni ya Samsung, Nationwide na Swedish betting company Svenska Spel.
Maisha binafsi;
John Terry amebahatika kupata watoto wawili ambao ni mapacha wa kike na wa kiume, huku mkewe wa ndoa Toni Poole Terry [40] mama wa mapacha hao Georgie John na Summer Rose ambao walizaliwa Mei 18, 2006.
Majiriwa ya kupata watoto hao, Terry aliweza kusherekea kwa kuifungia timu yake ya Uingereza dhidi ya Hungary .
Terry aliweza kufanya kufuli katika harusi yake, baada ya kufanya shamra shamra katika jumba la kifalme la Blenheim Palace , Juni 15, 2007 na kisha kukaa katika fungate kwa muda wa wiki mbili na malipo yote yakiwa juu ya Roman Abramovich.
Mshangao ;
Mwaka 2009, Terry aliweza kuchaguliwa kuwa mfano wa mzazi wa kuigwa ‘Baba wa mwaka wa mfano’ na kuonekana mtu muhimu kwa jamii kwa cheo hicho alichopata.
Lakini mwezi Januari 2010, vyombo vya habari vilimuandama na kusababisha kupelekana navyo Mahakamani.huku jaji mkuu wa Makhakama alipofungua kesi akipinga hatua za vyombo vya habari kumchonganisha Terry kuwa na mahusiano na Vanessa Perroncel ambaye ni mchumba wa zamani wa mwanasoka Wayne Bridge,aliyekuwa akichezea Chelsea na timu ya Taifa ya Uingereza.
Hata hivyo vyombo vya habari viliendelea kumuukumu kwa kitendo chake hicho, huku kwa kukusanya maoni mbalimbalai kwa wadau wa soka pamoja na mijadara hali ambayo ilisababisha kocha wake huyo wa timu ya taifa kuingilia kati swala hilo .
Kwa kukata mzizi wa fitina, Capello aliamua mnamo Februari 5, aliamua kumvua rasmi unahodha kwa kile alichokidai kuwa ‘Terry amebadilika kitabia huku akisisitiza kuwa kuwa kila mtu anamakosa yake kwa lililomtokera Terry linaweza kutokea kwa yoyote’ aliweza kutamka hayo Capello alipoojiwa na vyombo vya habari muda mfupi baada ya kutangaza kumvua unahodha kisha nkukabidhiwa Rio Ferdnand.
Kwa upande wa Terry swala hilo ahajalijutia sana zaidi aliweza kusema anakubaliana na maamuzi yaliyofikiwa, wadadisi wa mambo wanasemaa kuwa kwa kitendo cha Terry kumtaka kimada huyo atoe ujauzito, kimepelekea Uongozi wa FA na kocha Capello kumchinjia baharini Terry.
Kwa maoni; Mwisho
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa