Kijana huyu mkazi wa kibaha kijiji cha kidimu anashikiliwa na polisi kwa kosa la kumteka msichana wa kijijini hapo na kumfanya mateka wake.Binti huyo alipotea kwao kwa miezi minne na kupatikana juzi taehe 26 baada ya kupata upenyo na kutoroka.Hawa vijana wametoka Kigoma na walikuwa Kibaha wakitumika kama walinzi katika mashamba ya watu
Binti huyo alipotea hapo kijijini toka mwezi wa kumi na moja mwaka jana.Alishatafutwa kila kona ya kijiji hicho,waganga nao kupelekwa kuagua kuonyesha alipo mpaka manyau nyau alishafika huko.Wazazi walishaomba sana kanisani na kukata tamaa kuona kwamba kashakufa wakaweka na msiba kabisa.Kumbe alikuwa yupo kijijini akiwa kafichwa hapo kama uonavyo katika picha.
Kwa muda wote alkuwa akiishi kwenye hicho kichumba kama mke wa huyo kijana tena akiwa chini ya ulinzi mkali. Akapata na mimba kabisa ya miezi miwili wakamtoa kwa majani ya chai. Alipatikana juzi tarehe 26 baada ya kupata upenyo na kukimbia.
Hapa anaonyesha jinsi alivyokuwa akilala hilo eneo.
Vijana hao wanashikiliwa na polisi wapo watatu tayari kufikishwa mahakamani. Story zaidi endelea kusikiliza leo tena ya clouds fm kesho kupitia heka heka za leo.Leo ulisikiliza kiasi kesho pia itaendelea saa sita na nusu mchana.
CHANZO:kapingaz.blogspot.com
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa