Translate in your language

Sunday, April 18, 2010

MAN U YAIPUMULIA CHELSEA KILELENI KWA POINTI MOJA

Redhead alert

Manchester United's Paul Scholes
Getty Images

A stoppage-time header by Paul Scholes stunned rival Manchester City and kept Man United's EPL title hopes alive with a 1-0 road win.

 

LONDON, England

 

BAO pekee la sekunde ya 19 kabla ya filimbi ya mwisho, likifungwa kwa kichwa na Paul Scholes, jana liliwapa pointi tatu  mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya England, Manchester United, hivyo kuhuisha vita yao ya kutetea ubingwa wake ikifukuzana kwa karibu mshindani wake mkubwa, Chelsea.

Mechi hiyo iliyopigwa katika Uwanja wa Manispaa ya Manchester mbele ya mashabiki 47,019 na kuchezeshwa na mwamuzi Martin Atkinson, ilikuwa ya ushindani kwa dakika zote kutokana na kila timu kuhitaji ushindi kwani wakati United wakitaka kuongeza kasi ya kutetea ubingwa, Manchester City wanawania moja ya nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.  

Aidha, Manchester City ambao jana walikuwa nyumbani, walipambana vilivyo  kushinda mechi hiyo ili kulipa kisasi cha kufungwa mabao 4-3 katika mechi ya raundi ya kwanza, Septemba mwaka jana.

Matokeo yakiwa sare ya 3-3 hadi dakika ya 90, bao la dakika za majeruhi ambalo liliwekwa wavuni na Michael Owen, liliwafanya wenyeji Manchester United kubakisha pointi tatu nyumbani.

Katika mechi ya jana, bao la Scholes limeiwezesha United kufikisha pointi 76 ikiwa nyuma  pointi moja dhidi ya vinara Chelsea yenye pointi 77 ambayo jana ilishuka dimbani dhidi ya Tottenham.

Chelsea ilishuka dimbani ikitaka kushinda mechi hiyo ya ugenini ili kufikisha pointi 80, hivyo kuzidi kuikimbia United kuelekea ubingwa wa ligi hiyo iliyoanza Agosti 15, mwaka jana kwani baada ya mechi za jana, kila timu ikisaliwa na mechi tatu.

Scholes mwenye umri wa miaka 35, jana aliifungia United bao hilo la kichwa ikiwa ni siku moja tu tangu asaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuendelea kukipiga Old Trafford

Licha ya Scholes kubanwa na winga wa City, Adam Johnson, alifanikiwa kuupiga kichwa mpira huo na kujaa wavuni na kumwacha kipa Shy Given akiruka bila mafanikio.

Ligi hiyo itaendelea tena leo kwa mechi mbili ambapo Arsenal iliyo nafasi ya tatu kwa pointi 71, itakuwa wageni wa Wigan Athletic kwenye dimba la DW Stadium huku Portsmouth ikiwa mwenyeji wa Aston Villa.

 


No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)