Translate in your language
Sunday, September 10, 2017
Saturday, September 9, 2017
MASHINE ZA KUFYATULIA MATOFALI KUTOKA CHINA
katika kuunga juhudi za ukuaji wa uchumi wa viwanda, kampuni inayojishughulisha na biashara kwa njia ya mitandao (oreha) kwa kushirikiana na wadau wengine wanakuunganisha na kiwanda cha uzalishaji wa mashine za ufyatuaji wa matofali.
Mashine ambazo ni rahisi kwa matumizi na rafiki kwa matumizi ya mazingira yote (mjini na vijijini), Mashine za kufyatulia matofali ya udongo wa mfinyanzi na cement, tofali zinazoshikana/kuunganishwa zenyewe bila kuunganisha kwa cement/udongo (mota).
Mashine moja inaweza kuzalisha tofali/vigae vya aina tofauti kulingana na mahitaji yako, ni rahisi tu unakuwa unabadilisha moulds kulingana na aina ya tofali au kigae unachotaka
pia kwa wale watakaokuwa na mahitaji ya mashine tofauti na zinazoonekana katika picha wanakaribishwa kwa kuleta design/mchoro wa picha wanazozitaka na wakatengenezewa mashine katika ubora wa juu na zitakazoweza kukaa muda mrefu bila kuharibika na kufanya kazi katika ubora unaohitajika
Tofali imara zinazofyatuliwa bila kibao na kuweza kubebwa zenyewe kabla ya kukauka bila ya kuvunjika, Tofali zinazoweza kujengea nyumba imara na kwa bei nafuu sana.
Mashine ziko za aina tofauti na uchukua siku 30 hadi 45 toka ulipie mpaka kukufikia mkononi maana zinatoka china moja kwa moja.
Utaratibu wa malipo, tunaanza na malipo ya 30% kwanza kuanza matengenezo ya mashine kiwandani na kumalizia 70% inayobakia pale mashine yako inapokuwa imekamilika,
Mfumo wetu wa malipo ni mzuri na salama kwa pande zote mbili (mlipaji na mlipwaji). kwani ni mifumo ya kibenki (TT) inahusishwa kwa usalama zaidi wa fedha zako.
karibuni sana, kwa maelezo zaidi usisite kuwasiliana kwa namba zifuatazo:- 0783317009/0621108384 au kwa email orehabusuness@gmail.com
kama utahitaji kuona video jinsi mashine hizi zinavyoweza kufanya kazi ntumie whatsap message kupitia namba 0783317009 ukiandika "naomba ntumie video kuona inavyofanya kazi"
Sunday, September 3, 2017
Trailer Filamu Mpya ya 'The Life of Mad Man' Episode One imetoka
Inatia huruma sana maisha ambayo huwa wanaishi vichaa, kwani Maradhi, Chakula na Mavazi yao kiukweli Mungu ndio anajua hata afya zao pia, jiulize mara ya mwisho kumjulia hali kichaa ili kuwa lini?
Kwa mtu wa kawaida ni ngumu sana kujua uhalisia wa Maisha yao, sasa kupitia hii Filamu ya 'Maisha ya Kichaa' (The life of Mad Man) utafahamu maisha halisi ambayo huwa wanaishi Vichaa!. tupigie kwenye 0658161950 upate Orignal copy ya Episode One. Actor - Msanaki - Director Victor Petro tunaomba usapoti mabadiliko ya sanaa ya Tanzania asante "https://www.youtube.com/embed/z7ynNLPMjuw"
Friday, August 4, 2017
Mashine za kuulia na kufukuza mbu ndani ya nyumba
Kampuni yako ya OREHA inakuletea mashine za kisasa za kuulia na kufukuzia mbu zinazotumia umeme, na ambazo zina uwezo wa kudumu kwa takribani siku 60 (miezi 2) tangu kununua.
faida za mashine hizi:
1. Zinakuja na tofauti na dawa, hivyo unaweza ukanunua dawa pale inapoisha na kuendelea kutumia mashine yako
2. Haugombani na watoto pale wanapoacha mlango wazi, dawa inakuwezesha kuwepo katika chumba/nyumba kwa kipindi chote inapokuwa inawaka
3. Unaweza pia kusafiri nayo (portable) kama unakoenda kuna chanzo cha umeme
4. Inakula umeme mdogo sana ambao hauwezi kukuathiri katika matumizi yako ya LUKU
5. Haina madhara kwa binadamu (wakubwa na wadogo)
6. Ni rafiki kwa mazingira (haitoi moshi, wala harufu mbaya)
7. Haiitaji kukaa nje wakati wa kuweka kama vile dawa za kupulizia
8. Ni rahisi kutumia, unachomeka katika umeme na kuwasha tu
9 Inaweza kutumia kama marembo ndani ya nyumba
10. Inaweza kutumika kama chanzo cha manukato ndani ya nyumba (air fresh)
Bei: ni sawa na kutupa, inapatikana kwa kiasi cha shilingi 12,000/= tu ikiwa ni gharama ya mashine na dawa, na shilingi 6,000/= kama utaitaji dawa peke yake, karibuni sana
Huu ndio muonekano wake |
Muonekano wa boksi wa mashine tulizonazo kwa sasa |
Aina nyingine za muonekano wa mashine |
Inatumia Umeme |
Aina ingine tuliyonayo kwa sasa |
Dawa yake (re fill) zinapatikana kwa wingi, ziko aina tofauti (zilizo na harufu (manukato) na zisizo na manukato |
KARIBUNI SANA, KWA DAR ES SALAAM UKIAGIZA KUANZIA TATU (3) TUNAKULETEA MPAKA NYUMBANI/OFISINI, KWA MIKOANI TUNATUMA KWA GHARAMA ZA MTEJA
Wednesday, March 15, 2017
Dk. Kigwangalla aongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano wa CSW 61
Dk. Kigwangalla aongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano wa 61 wa Kimataifa wa Kamisheni ya hali ya Wanawake Duniani
NEW YORK: Naibu Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mheshimiwa Dkt. Hamisi Kigwangalla (Mb) ameongoza ujumbe wa Tanzania wa wizara zinazohusika na mambo ya uwezeshaji wa wanawake kiuchumi za Tanzania Bara na Zanzibar juu ya uwezeshaji wa Wanawake Waliopo kwenye sekta isiyo rasmi, mjini New York City, Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, kwenye Mkutano wa 61 wa Kimataifa wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani.
Katika hotuba yake katika mkutano huo wa Mawaziri wa Wanawake Duniani, Dk. Kigwangalla ameeleza mambo mbalimbali ikiwemo hatua tulizofikia kama nchi kwenye kuleta usawa wa kijinsia na ukombozi wa mwanamke wa kitanzania hususani kiuchumi ikiwemo vikwazo vya kimila vinavyomfanya mwanamke kuwa wa hali ya chini kwenye jamii, pamoja na changamoto anazokumbana nazo mwanamke kwenye ajira zisizo rasmi (informal sector) ambapo wanawake ni wengi (asilimia 82) ukilinganisha na wanaume (asilimia 72).
"Ilikufikia malengo, Jitihada za serikali za nchi yetu kuanzia kuweka usawa wa kijinsia na kupinga ubaguzi kuanzia kwenye katiba yeti, sera ya mikopo midogo midogo, sheria zinavyoweka sharti la mali za wanandoa kutowekwa dhamana ama kuuzwa kama mwanandoa mmoja hajaridhia, uanzishwaji wa mfuko wa maendeleo ya wanawake kwenye halmashauri zote 114 Tanzania bara ambapo asilimia 5 ya bajeti ya mapato ya ndani ya halmashauri ni lazima iende kwa wanawake.
Pia jitihada tunazofanya kuwahamasisha wanawake wamiliki mali, warasimishe biashara zao (Mkurabita), pia waraimishe vikundi vyao vya kuweka akiba na kukopa na vya kusaidiana" Ameeleza Dk. Kigwangalla kwenye mkutano huo.
Aidha, Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, kwa upande wa Tanzania, Serikali imepiga jitihada kubwa kuhakikisha inamkomboa mwanamke kutoka kwenye utegemezi kwa kuunda vyombo mbalimbali na kuandaa sera na miongozo inayoelekeza usawa katika kufikia malengo ya kumkomboa mwanamke kiuchumi ambapo mwanamke anakuwa na haki na uwezo wa kukopa katika taasisi mbalimbali ili kuanzisha au kukuza mtaji wa biashara yake katika kufikia malengo aliyotarajia.
Vile vile imeanzisha mfuko wa maendeleo katika halmashauri zote 114 nchini ili kuwafikia wanawake walio wengi zaidi, imeendelea kuhamasisha Jamii kuanzisha mifuko mbalimbali ya kuweka na kukopa kama vile (VIKOBA) , kuwahamasisha kushiriki katika maonyesho mbalimbali ya kitaifa na hata mikutano mikubwa ya kimataifa ili kujitangaza na kukuza bidhaa mbalimbali kwa lengo la kujipatia kipato na kukuza mitaji yao.
Ameongeza k uwa, kufanya hivyo, kunawasaidia kutengeneza mitandao ya kibiashara itakayowasaidia kukua kimataifa na kufanya biashara Kubwa za kimataifa na pia kutoa ajira kwa Wanawake wenzao . Pia Serikali imeanzisha benki ya Wanawake ambayo Kazi yake Kubwa ni kutoa mikopo na ushauri ambao utawasaidia kukuza biashara zao na kuongeza kipato kwani Wanawake ni Jeshi kubwa ambalo linachangia uchumi wa nchi kwa kiasi kikubwa.
Kampuni ya Quality Group LTD yaelezea mipango mipya ya miradi yake nchini
Kampuni ya Quality Group LTD yaelezea mipango mipya ya miradi yake nchini
Mkurugenzi Mkuu wa makampuni ya Quality Group Limited, Bwana. Nicholas Ralph leo Machi 15.2017, amekutana na vyombo vya habari na kuelezea mipango mbalimbali ya kampuni hiyo ikiwemo miradi yake inayoendeshwa karibu nchi nzima Tanzania Bara na Visiwani.
Akizungumza na vyombo mbalimbali katika tukio lililofanyika majira ya Alasiri ya leo Machi 15, Mkurugenzi huyo ameweza kuweka bayana miradi yao hiyo pamoja na muelekeo wa kampuni katika kufikia malengo yake huku akibainisha kuwa, wataendelea kufanya kwa kiwango cha hali ya juu ikiwemo kuwafikia wananchi kama sera ya makampuni hayo na ile ya Taifa huku wakiungana na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli ya kupiga vita rushwa na kuifanya Tanzania ya Viwanda.
Akielezea muelekeo wa kampuni hiyo amebainisha kuwa watanzania wanaimani nao hivyo wataendelea kujikita zaidi kwenye miradi na kuwafikia watanzania sehemu mbalimbali kama dira yao ya kuiletea Tanzania maendeleo yaani 2016/2021 na ile ya mpaka 2025
"Quality Group imeweza na inaendelea kushirikiana na makampuni yenye majina makubwa Duniani kwa kufanya nao kazi pamoja na uwakala kwa hapa Tanzania ikiwemo kampuni za GM, Hoda,Isuzu, Bridgestone pamoja na Chevrolet huku yakizalisha faida maradufu hii ni pamoja na kutoa ajira kwa watanzania" amesema Mkurugenzi huyo.
Aidha, akitaja baadhi ya miradi ambayo inasimamiwa na kampuni hiyo hapa nchini ni pamoja na mradi wa shamba la mpunga lililopo Mkoani Morogoro ambalo litakuwa likipanda mazao hayo sambamba na kununua kwa wakulima wadogowadogo ili kupata mchele.
Quality Group pia inasimamia miradi Visiwani Zanzibar ikiwemo ule wa Stone Town Village huku pia mirad mingine ni ule wa Matrekta ambao ni wa Sonalika.
Kampuni hiyo kwa hapa nchini ni ya miaka mingi zaidi ya miaka 30 huku ikiwa imeweza kuajili wafanyakazi zaidi ya 667,300 huku ikitengeneza zaidi ya faida Bilioni 348.6 huku wa miongoni mwa makampuni bora na yenye majina makubwa kwa kujijengea heshima ndani na nje ya nchi.
Saturday, March 4, 2017
CDEA yawapiga msasa wabunifu wa mavazi na urembo wa Afrika Mashariki kwa ufadhili wa IIDEA 2017
CDEA yaendesha mafunzo ya IIDEA 2017 kwa wabunifu mavazi na urembo wa Afrika Mashariki
Wabunifu wa mavazi na urembo kutoka nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania na Uganda, wamepigwa msasa wa namna ya kuendesha na kukuza fani zao kwenye sekta za ubunifu na biashara IIDEA 2017,mafunzo yaliyoandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali (Culture and Development East Africa -CDEA) la jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuongeza ujuzi na elimu ya biashara pamoja na masoko ambapo mafunzo hayo yanafadhiliwa na GIZ tawi la Afrika Mashariki.
Awali akizungumza katika mafunzo hayo ambayo yalikuwa ya siku nne, Mkurugenzi Mtendaji wa CDEA, Bibi Ayeta Wangusa alishukuru na kuwapongeza washiriki kwa kuchaguliwa kwenye mradi huo ambao ni wa kwanza na wa kipekee katika ukanda wa Afrika Mashariki huku ukiwa chachu katika kuinua uchumi kwa kupitia sekta ya ubunifu huku akiwataka washiriki hao kuzingatia yale yote watakayofundishwa hususani suala la kutafuta masoko nje ya mipaka ya nchi zao wanazotoka.
Mafunzo hayo yalihusisha jumla ya ya washiriki 17 ambao walibahatika kuchaguliwa waliweza kujengewa uwezo na mbinu mbalimbali ikiwemo zaUbunifu wa mavzi, Biashara, Mtandao, Sheria na mbinu tofauti za kupata ufadhili.
Aidha, miongoni mwa walimu waliotoa mafunzo hayo, wakiwemo Bibi Santa Anzo na Bibi.Bernadine Buzabo kutoka nchini Uganda, waliweza kutoa mafunzo na mbinu za ubunifu na kufanya mauzo ya kazi zao ikiwemo kwenye masoko tofauti ya ndani na nje ikiwemo Afrika, Ulaya na Amerika.
Washiriki hao pia walipata wasaha wa kujifunza namna ya kuandaa Mpango wa kazi zao za biashara na usajiri wa biashara ikiwemo kusajiri kampuni pamoja na kujitengenezea majinna (branding).
Mafunzo hayo ya siku nne, yaliwawezesha washiriki kupata wasaha wa kutumia bidhaa halisi za ndani ya nchi za Afrika Mashariki ikiwemo khanga zilizotengenezwa na pamba ya hapa nchini Tanzania, Ngozi halisi ya mbuzi, Shanga na simbi ambazo zitokanazo na zao la baharini ambazo pia zilikuwa kivutio katika kazi zao hizo.
Kwa upande wao waratibu wa mafunzo hayo, wamebainisha kuwa,wamedhamilia kutumia bidhaa za asili ili kukuza uchumi katika ngazi zote za mnyororo wa thamani katika sekta ya ubunifu wa mavazi na mitindo.
Mradi huo pia unajulikana kama Atamishi ya kazi za Sanaa (IIDEA) unaratibiwa na CDEA kwa ufadhili wa GIZ East Africa, ukiwa na lengo la kukuza ujuzi na elimu ya biashara kwa sekta ya filamu, muziki na ubunifu wa mavazi huku kwa sasa ukihusisha nchi mbili za Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania na Uganda.
Kwa sasa mafunzo hayo ya Atamishi ya kazi za Sanaa (IIDEA) yameanza na masuala ya ubunifu wa mavazi na urembo ambapo pia yatafuatiwa na mafunzo mengine ikiwemo Muziki na filamu.
Tazama hapa matukio mbalimbali ya picha ya mafunzo hayo:

Washiriki ambao ni wabunifu kutoka Afrika Mashariki akiwemo Andrew Kalema, Joyce Gerald (katikati) na Makeke Jocktan wakifuatilia mafunzo hayo
Washiriki na wataalamu wakibadilisha mawazo wakati wa semina magunzo hayo
Bi Amal Mohamed kutoka Kenya akitoa mafunzo ya namna ya kupata Ufadhili kupitia ubunifu kwa wabunifu wa Afrika Mashariki
Bi Bernadine Buzabo akiwasilisha mafunzo kwa washiriki kwa njia ya mtandao wa Skype kwa washiriki (Hawapo pichani)
Mtendaji Mkuu wa CDEA, Bibi Ayeta Anne Wangusa akitoa takwimu za fashionomics kwa washiriki wa mafunzo hayo
Mmoja wa wanufaika wa ufadhili kupitia ubunifu kutoka Kenya Bwana James Otieno akitoa mafunzo kwa washiriki
Baadhi ya washiriki Ester Kiula na Whitnery Gnaj wakifuatilia mafunzo hayo
Mshiriki kutoka Uganda, John Okello akishona vazi alilobuni mwenyewe wakati wa mafunzo hayo
Kemi Kalikawe kutoka Tanzania akipitia mchoro wa mshiriki Clare Musila (Uganda) wakati wa mafunzo hayo
Mshiriki akimuonesha mkufunzi kazi yake namna ya inavyovaliwa
Mshiriki akipata maelekezo ya vipimo toka kwa mkufunzi
Kemi Kalikawe akimuelekeza Catherine Mood Board
Mshiriki Victoria Joseph akiwa kwenye ubunifu wake
Kebirugi Nina akishona vazi alilobuni
Whitney Gnaj akijaribu vazi alilolibuni
Kemi Kalikawe akipitia mchoro wa Clare Musila
Wakili masuala ya miradi na biashara Bi. Sia Mrema akifundisha kuhusu usajili wa biashara na makampuni kwa washiriki hao ili kujitangaza zaidi hasa kupitia majina yao ya ubunifu (brand).
Bibi Santa Anzo ambaye ni mbunifu mkongwe na mahiri nchini Uganda akitoa mafunzo ya namna ya wabunifu watakavyoweza kubuni ubunifu wao na kuuza bidhaa zao katika masoko ya nje.
Aliyewahi kuwa Miss Tanzania kipindi cha nyuma, Bi. Nasreen Karim akipitia kazi ya mwanafunzi Clare Musila
Aliyewahi kuwa Miss Tanzania kipindi cha nyuma, Bi. Nasreen Karim akitoa mafunzo kwa wabunifu hao (Hawapo pichani) wakati wa mafunzo ya IIDEA 2017.
Mmoja wa walimu wakitoa mafunzo katika mafunzo hayo.
Vazi la mbunifu wa Tanzania Makeke Jocktan alilolibuni wakati wa mafunzo hayo.
Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo
Wabunifu wakiendelea na ubunifu wao
Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo
Baadhi ya vitu vilivyotengenezwa na wabunifu hao katika mafunzo ya IIDEA 2017

Kazi za wabunifu zilizofanywa na washiriki
Baadhi ya washiriki wabunifu na walimu wakipiga picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu wa CDEA, Bibi Ayeta Anne Wangusa.
Picha ya pamoja ya washiriki wote wakipiga baada ya kumaliza mafunzo hayo ya IIDEA 2017.