Kampuni ya Multichoice Tanzania wasambazaji wa visambuzi vya kisasa vya DSTV mapema jana 28 Desemba 2016, wametoa zawadi ya msimu wa Sikukuu kwa wadau wao mbalimbali ikiwemo kwa mwandishi Mwandamizi wa mtandao (Blog) wa MODEWJIBLOG, Ndugu Andrew Chale.
Akikabidhi zawadi kwa niaba ya uongozi wa kampuni hiyo ya Multichoice Tanzania, Costomer Retention Representative, Vida Msuya aliipongeza MO BLOG pamoja na mwanahabari huyo kwa kuwa mstari wa mbele katika kuitangaza vyema DSTV kwa muda wote, na zawadi hiyo ni moja ya kurudisha fadhila kwa wadau wao.
"Lengo la DSTV ni kuona tunazidi kuwa na wateja wengi ambao pia wanapata kitu bora kutoka kwetu. Huduma zetu nzuri na za kisasa hivyo kwa msimu huu wa Sikukuu wateja wetu na wadau tunawatembelea na kuwapatia zawadi." Alieleza Vida Msuya.
Aidha, DSTV pia imeweza kuwapatia wadau mbalimbali zawadi hizo za Sikuukuu na kuwatakia kheri ya Mwaka mpya wa 2017.
Aidha, kupitia kwa Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Bw. Alpha Joseph hivi karibuni amebainisha kuwa katika msimu huu wa kusherehekea Sikukuu ya christmas na mwaka mpya wateja wao watapata kuangalia chaneli zaidi ya 70 za DStv ikiwemo mpira wa ligi ya Hispania (Laliga) na ligi ya Uingereza na zingine nyingi huku wakishusha bei za vifurushi vyao kwa wastani wa asilimia 16, kifurushi maarufu cha DStv Bomba chenye chaneli zaidi ya 70 kikipunguzwa bei hadi sh.19,975 tu kwa mwezi.
No comments:
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa