Thursday, October 6, 2016

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe Deogratius Ndejembi akishiriki katika zoezi la kuvuruga bustani ambazo zimelimwa karibu na vichoteo vya maji kwa ajili ya matumizi ya wananchi.




Na Mathias Canal, Dodoma



Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe Deogratius Ndejembi ameshiriki katika
zoezi la kuvuruga bustani ambazo zimelimwa karibu na vichoteo vya maji
kwa ajili ya matumizi ya wananchi.



Dc Ndejembi ameamua kufanya zoezi hilo la kuharibu bustani hizo baada
ya wananchi Karibu na vyanzo hivyo vya maji baada ya wananchi wanaoishi
karibu na maeneo hayo kuamua kulima bustani za mboga mboga kwa kutumia
maji ya bomba ambayo hupaswa kusukumwa kujaza tanki la kutunzia maji.



Uharibifu huo umefanywa na Dc Ndejembi huku akiwa ameongozana na Kamati
ya Ulinzi na usalama ya Wilaya ya Kongwa ikiwa ni sehemu ya utendaji
Kazi na kuhamasisha ufanisi wa ukuzaji wa kilimo chenye tija.



Dc
Ndejembi ameamua kufanya hivyo baada ya kubaini kuwa wananchi hao
wamekuwa wakifungulia maji ya bomba na hatimaye kumwagika chini ili
kumwagilia bustani zao nyakati za usiku muda ambao pampu inasukuma maji
kuelekea kwenye Tanki lililopo makao makuu ya Wilaya ambalo hujazwa ili
maji hayo yaweze kuwahudumia wakazi wa Mjini Kongwa.



Kadhia hiyo
ya kufunguliwa maji kwa kificho nyakati za usiku imesababisha kutojaa
kwa Tanki hilo Hali ambayo imesababisha kukosekana kwa maji katika
maeneo ya Wilaya ya Kongwa.



Kabla ya kuanza kwa zoezi hilo la
kuvuruga bustani hizo Dc Ndejembi aliamuru wananchi waliohudhuria katika
zoezi hilo kuchuma mboga mboga zilizokuwepo katika bustani hizo
sambamba na kuchota maji yote ambayo yalikuwa yamehifadhiwa katika
bustani hizo kwa ajili ya kumwagilia bustani hizo.



Vichoteo
vilivyotobolewa katika bomba kuu ambalo linalekea Mjini vipo katika
kijiji cha Ibwaga ambavyo vilianzishwa maalumu kwa ajili ya kusaidia
wanakijiji wa vijiji vya karibu

No comments:

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa