Waratibu wa elimu wakisikiliza kwa makini maelekezo ya utendaji kazi kutoka kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi kayombo
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi kayombo akisisitiza jambo wakati wa kikao cha pamoja na waratibu wa elimu Kata wakati wa kikao cha Kazi
Watumishi wa Manispaa ya Ubungo wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi kayombo wakati wa kikao cha kazi
Watumishi wote wanaofanya kazi katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo
wametakiwa kufanya kazi katika hali ya ukweli, Uwazi, Ufanisi,
Uadilifu, Kujituma na kuwa na nidhamu katika utendaji ili kukuza ufanisi
wa Changamoto zinazowakabili wananchi mbalimbali.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam
Ndg John L. Kayombo wakati wa kikao cha kazi na waratibu wa elimu
kutoka kata 14 na wakuu wa shule za msingi zilizopo katika Manispaa hiyo
mara baada ya ukaguzi wa shule za msingi Temboni Msigani.
Kayombo amezuru katika maeneo tofauti tofauti katika Halmashauri hiyo
ikiwemo Shule ya Msingi Temboni ambapo alikutana na kamati ya shule
sambamba na kufanya ukaguzi wa vyumba 8 vya madarasa utakaogharimu kiasi
cha Shilingi milioni mia moja sitini (Mil 160) na matundu kumi ya choo
ambayo yanataraji kugharimu kiasi cha shilingi milioni thelathini na
mbili (Mil 32) ambapo pia ukarabati wa shule wenyewe utagharimu kiasi
cha shilingi milioni kumi (Mil 10).
Kayombo alisema kuwa fedha
hizo zimetolewa na serikali kuu kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu na
kuhakikisha watoto wa masikini wanapata elimu bora katika mazingira
rafiki.
Ziara ya kazi ya Mkurugenzi huyo wa Manispaa ya Ubungo
John L. Kayombo kwa kukutana na waratibu wa elimu kutoka kata 14 za
Halmashauri hiyo pamoja na wakuu wa shule za msingi imejikita zaidi
katika kuamsha ari na ufanisi katika utendaji na kuwakumbusha watendaji
wote majukumu yao ya kuwatumikia wananchi.
Ziara hiyo inatazamiwa
kuwa kila mtumishi sasa atakumbuka majukumu yake katika utendaji na
kuyafanya ipasavyo kwa mujibu wa kanuni, taratibu na sheria za muongozo
wa watumishi wa umma.
Akizungumza na www.wazo-huru.blogspot.com
DED Kayombo alisema kuwa watumishi wa serikali wanapaswa kutambua kuwa
hawatakiwi kujiingiza na kufanya siasa zisizo na tija badala yake
wanapaswa kuwajibika zaidi katika kuwatumikia watanzania na kuakisi
kauli mbiu ya serikali ya awamu ya tano ya Hapa Kazi Tu chini ya Rais
Dkt John Pombe Magufuli.
Kuzuru katika maeneo mbalimbali kukagua
miradi na kujionea shughuli za maendeleo ni utaratibu ambao amejiwekea
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo John L. Kayombo ili
kufahamu maeneo yake ya kiutendaji na kuamsha ari katika uwajibikaji na
ufanisi wa kazi.
Baada ya ziara hiyo ya kukutana na waratibu Kata katika Manispaa ya Ubungo DED Kayombo hii leo amekutana tena na watumishi wote wa Manispaa kikiwa ni kikao chake cha kwanza kukutana na Watumishi wote kwa lengo la kutoa miongozi na maelekezo mbalimbali katika utekelezaji wa majukumu yao.
Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Manispaa ya ubungo Mkurugenzi huyo amesisitiza ufanyaji kazi kwa bidii, ushirikiano mahali pa kazi, upendo na uaminifu ili kuiwezesha ubungo kusonga mbele katika maendeleo na kuwafanya wananchi wa Ubungo kuimarika katika sekta ya uchumi.
DED Kayombo amewataka watumishi hao kuwa wabunifu katika utendaji kazi wao ili kuongeza mapato ya ya manispaa ya kurahisisha Manispaa hiyo katika ufanisi wa kazi na kuwahudumia wananchi kirahisi.

No comments:
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa