Friday, May 6, 2016

ZIFF 2016 Announces Film Selection with Strong East African Presence


__________________________________________________________________

Tamasha la filamu la Zanzibar (ZIFF) limetangaza majina ya filamu zitakazoshindanishwa hapo ifikapo Julai 9 hadi 17. Tamasha lilipokea jumla ya filamu 490 kutoka nchi 32 mwaka 2016.

Jopo la wachaguzi limependekeza filamu 80 ndio zitakazoshindanishwa katika makundi matano maalum: Kundi la Kawaida 59, Sembene Ousmmane 15, filamu 12 Bongo movies.  Nyingine 5 ni la kundi jipya kabisa la filamu zinazoizungumzia Zanzibar itakayopata tuzo ya Emerson.

Kutakuwepo pia mashindano ya Video za Muziki ambazo zitatangazwa mwisho wa mwezi Mei na hizi zitaoneshwa katika maonyesho yanayofanyika katika Ngome Kongwe.

Jambo la kukumbukwa zaidi mwaka huu nikuongezeka kwa jumla ya filamu za kitanzania katika mashindano. Filamu zaidi ya 40 zilitumwa kwa mashindano kwa ujumla na mwaka huu filamu 5 za kitanzania zitashindanishwa katika jopo la Ousmane Sembene kati ya filamu 17.

Kwa ujumla filamu toka Afrika mashariki zinazoingia katika mashindano zimeongezeka pia ambapo kuna 8 toka Tanzania, Kenya 5, Uganda 3 na Rwanda 2.


Mwaka huu kutakuwa na filamu 3 ambazo zitaoneshwa kwa mara ya kwanza duniani  katika tamasha la ZIFF. Filamu hizi zimedhaminiwa na Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Ujerumani (GIZ) wakishirikiana na ZIFF. Washindi watatu wa shindano la Sembene Ousmane mwaka 2015 walipewa $2000 kila mmoja kuwawezesha kutengeneza filamu mpya katika kipindi cha mwaka na kuzituma tena ZIFF kwa kushindanishwa na nyingine.

Mvuto wa tamasha unazidi kukua ukiangalia kuongezeka kwa nchi zinazotuma filamu. Mwaka huu Estonia na Albania zimetuma filamu zikiungana na nchi nyingine kama Bangladeshi, Finland, Trinidad and Tobago, Bermuda na nyinginezo.

ZIFF pia inaendeleza mchango wake katika tasnia ya filamu kwa kutayarisha warcha maalum juu ya utengenezaji filamu. Mwaka huu ZIFF imetangaza warsha mbili. Ya kwanza ni juu ya matumizi bora ya Camera ya Canon D5 itakayoendeshwa na Barry Braverman toka Marekani ,aliyeifanyia kazi Panasonic na Sony katika kujaribisha vifaa vyao.

Warsha nyingine ni ile itakayodhaminiwa na Goethe Institute ya Ujerumani itayofunza watoto wa shule ufundi wa kutengeneza vikaragosi katika filamu. Hii inatokana na kutambua nafasi ya sanaa katika kukuza vipaji na kuwatayarisha watoto wasanii kwa ajira, uadilifu na ubunifu.

Kwa maelezo zaidi na kupata listi ya filamu zilizochaguliwa tembelea tovuti ya www.ziff.or.tz  na pia tafadhali tu-like katika Facebook

No comments:

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa