Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imebainisha kuwa itaendelea kushirikiana na taasisi binafsi katika kuleta maendeleo kwenye nyanja mbalimbali hapa nchini huku ikipongeza juhudi zinazofanywa na Taasisi ya mtandao ya Aga Khan kwa jitihada zake kufundisha wataalam wa sekta ya Afya.
Kauli hiyo imetolewa leo Machi 31.2016 na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati wa ufunguzi rasmi wa jengo la shule ya Uuguzi na Ukunga katika ngazi ya digrii katika chuo cha Aga Khan, Jijini Dar es Salaam.
Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, Chuo hicho Kikuu cha Aga Khan kwa kuanzisha shule hiyo wanaongeza idadi ya vyuo vitakavyokuwa vikizalisha kwa wingi wataalam watakaokuwa wakipta digrii kwani awali kulikuwa na upungufu mkubwa.
Jengo la Chuo hicho cha Uuguzi na Ukunga, limefanyiwa ukarabati pamoja na kupatiwa vifaa mbalimbali kwa msaada wa Serikali ya Ujerumani kwa ushirikiano na Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo waliwezesha kwa kugharamia ujenzi wa jengo hilo pamoja na vifaa vya kisasa vya kufundishia.
Kwa upande wake, mgeni rasmi mwakilishi wa Serikali ya Ujerumani, Waziri wa Uchumi na Maendeleo, Dk. Gerd Muller ambaye alibainisha kuwa, wanataka kuona watalaama wengi wa sekta ya afya wanapata elimu ilikuondokana na matatizo mbalimbali yanayowakabili wanadamu na kuongeza kuwa, bila wataalam wa tiba, Jamii haitakuwa salama.
Aidha, katika tukio hilo,wageni na viongozi mbalimbali walipata kulitembelea jengo hilo pamoja na kushuhudia shughuli mbalimbali zilizokuwa zikiendelea shuleni hapo.
Tazama MO tv, kuona tukio hilo hapa:
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wageni mbalimbali waliojumuika katika tukio hilo la ufunguzi rasmi wa jengo la shule ya Uuguzi na Ukunga ngazi ya digrii katika Chuo Kikuu cha Agha Khan, Upanga jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akifurahia jambo na Waziri wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani, Dkt. Gerd Muller na wageni mbalimbali waliojumuika katika tukio hilo la ufunguzi rasmi wa jengo la shule ya Uuguzi na Ukunga ngazi ya digrii katika Chuo Kikuu cha Aga Khan, Upanga jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi na watumishi wa Chuo hicho wakiwa katika tukio hilo
Waziri wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani, Dkt. Gerd Muller akisisitiza jambo..
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akisisitiza jambo..
Waziri wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani, Dkt. Gerd Muller akitoa maelezo mafupi kabla ya kuzindua rasmi jengo hilo la shule ya wauguzi na wakunga katika chuo kikuu cha Agha Khan..
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa hotuba ya Serikali namna Wizara Afya itakavyonufaika na wataalam wa sekta ya Afya watakaopata elimu katika shule hiyo
Waziri wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani, Dkt. Gerd Muller akifungua rasmi jengo hilo
Wageni mbalimbali wakifuatilia tukio hilo
Msimamizi wa shule hiyo ya Uuguzi na Ukunga akitoa maelezo machache kwa wageni mbalimbali..
Picha ya pamoja baada ya ufunguzi huo..
Waziri wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani, Dkt. Gerd Muller akiangalia namna ya vifaa vya kisasa vya kufundishia jinsi viavyotumika wakati wa kutoa huduma Hospitalini
Waziri wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani, Dkt. Gerd Muller akijaaribu kupata vipimo kuashiria ufunguzi wa jengo hilo pamoja vifaa vya kisasa vilivyowezeshwa na Serikali ya Ujerumani. Kushoto kwake ni Dk. Kigwangalla akimwelezea jambo la kitaalam juu ya vipimo hivyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari namna Serikali itakavyonufaika kupitia shule hiyo. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog).
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imesema kuwa ipo tayari kushirikiana na wadau mbalimbali akiwemo Mwanadada Millen Magese na Taasisi yake katika mapambano ya ugonjwa na athari za Endometriosis ambao unawapata wanawake wengi hapa nchini.
Kauli hiyo imetolewa mapema leo Machi 30.2016 na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati wa kufungua rasmi semina maalum kwa vijana wapatao 500 wa shule za Sekondari zikiwemo za Turiani Sekondari, Makurumla na zinginezo za Manispaa ya Kinondoni pamoja na walezi na walimu, ambapo katika mkutano huo, Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, juhudi zinazofanywa na Mwanadada Millen Magese ni za kuungwa mkono hivyo wataendelea kushirikiana naye bega kwa bega.
Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, anatambua wanawake wengi duniani kote wanasumbuliwa na tatizo hilo ambapo gharama zake kwa kawaida ni kubwa huku bado wataalam wanaendelea kushughulikia namna ya upatikanaji wa tiba yake ili kuweza kuwa nafuu.
“Napongeza juhudi za dhati zinazofanywa na taasisi ya Millen Magese, katika kuunga mkono juhudi za serikali ya tano kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto za kuwasogeza wananchi karibu na huduma bora kwa ajili ya Maendeleo na Ustawi wa Jamii yetu.
Tatizo la kutoshika mimba (kitaalamu Endomytiosis) hutokana na sababu mbalimbali, nyingi zikichangiwa na uelewa mdogo wa jamii inayomzunguka msichana au mama anayejianadaa kuanza kubeba mimba, lakini pia upungufu wa vifaa tiba hospitalini na kwenye vituo vya afya sambamba na kukosekana kwa wataalamu katika hospitali zetu, Hivyo tunapenda kuchukua fursa hii kupongeza juhudi kama hizi za kuandaa semina na warsha ikiwa ni hatua madhubuti na ya msingi katika kuikabiliana na changamoto ya uelewa wa tatizo hili katika jamii.
Kwani, tunaamini, limekuwa jambo la faraja sana, tangu Magesse alipojitokeza hadharani na kuihabarisha dunia juu ya tatizo hili linalomkabili yeye binafsi. Naomba kusema wazi kuwa, huo ulikuwa uthubutu wa pekee wa mrembo huyo, kiasi cha kuifanya jamii kubwa ya kimataifa kuanza kulifuatilia tatizo hili ili kusaidia mabinti wadogo ambao walikuwa hawajakumbwa na hali hiyo. “ alieleza Naibu Waziri Dk. Kigwangalla katika hotuba yake hiyo.
Aidha, Dk. Kigwangalla aliongeza kuwa, ni faraja kubwa kwa watanzania tangu Magese Foundation ilipoanzishwa ikifanya kazi kubwa ya kuhamasisha upatikanaji wa vifaa na pia ujenzi wa hospitali maalumu kwa ajili ya kutibu tatizo hilo. Jambo hilo linaendelea kuitia moyo serikali hususani Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kufikia lengo la kumuwezesha mtoto wa kike kufikia malengo tarajiwa.
Kwa upande wake, Mwanadada Millen Magese amewaeleza vijana wa kike katika semina hiyo kuwa, wawe wazi pindi wajisikiapo dalili mbalimbali wakati wanapokuwa katika mzunguko wa siku zao ambapo na kubainisha kuwa, jambo hilo endapo litabainika mapema ni rahisi kulipatia tiba kuliko kuficha na kufika steji mbaya.
Mwanadada, Millen Magese pia alitumia wasaha huo kuishukuru Serikali kwa namna walivyokubaliana kushirikiana naye bega kwa bega katika mapambano dhidi ya tatizo hilo hapa nchini ambapo pia amewashukuru wadau wote kwa kuwa naye dhidi ya mapambano hayo.
Semina hiyo pia imeweza kukusanya watu mbalimbali wakiwemo watu maarufu wasanii, wanamitindo na wabunigu wa mavazi, wafanyabiashara na wanaharakati wanawake katika maendeleo hapa nchini huku wanaume nao wakijumuika pamoja ilikusambaza ujumbe huo kwa wenza wao na marafiki zao.
Tazama MO tv, kuona tukio hilo hapa:
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (wa kwanza kushoto) akifuatiwa na Mwanadada, Millen Happiness Magese (katikati) pamoja na Afisa Elimu Manispaa ya Kinondoni, Bw. Rogers Shemwelekwa.
Mwanadada, Millen Happiness Magese.
Baadhi ya wanafunzi, wadau wanaosaidiana na mwanadada Millen Magese wakifuatilia semina hiyo.
Baadhi ya wageni waalikwa, wakiwemo waliowahi kushiriki mashindano ya ulimwende hapa nchini ..wakiwa wamejumuika pamoja kuungana na taasisi ya Millen Magese.
Wanafunzi wakifuatilia semina hiyo
Wanafunzi wakifuatilia semina hiyo.
Afisa Elimu Manispaa ya Kinondoni, Bw. Rogers Shemwelekwa akitoa hotuba fupi katika semina hiyo
Baadhi ya wadau walioungana kwa pamoja kusaidiana na taasisi ya Millen Magese wakifuatilia semina hiyo. Mustafa Hassanali pamoja na Rio Paul ambao wote ni wabunifu wa mavazi hapa nchini.
Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni,akitoa hutuba yake
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa hutuba yake katika semina hiyo.
Mmoja wa madaktari bingwa wa wanawake wa Hospitali ya Muhimbili akitoa maelezo machache .
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akifuatilia mjadala huo uliokuwa ukiendeshwa kwenye semina hiyo..
Mwanadada Doris Mollel ambaye alikuwa akiongoza semina hiyo akieleza machache wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi Dk. Kigwangalla.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa maelezo machache wakati wa kufunga mkutano huo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla na Mwanadada Millen Happiness Magese wakipata picha ya pamoja na wanafunzi wa shule za Sekondari mara baada ya kumaliza kwa mkutano huo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akipiga picha ya pamoja na Mwanadada Millen Magese.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akipata picha ya pamoja na wanafunzi hao.
Mwanadada Millen Magese akipata 'Selfie' na wanafunzi pamoja na mgeni rasmi Naibu Waziri Dk. Kigwangalla
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla na Mwanadada Millen Magese wakifurahia jambo na wanafunzi
Mwanadada Millen Magese akipata picha ya 'selfie' na wanafunzi waliojumuika katika semiana hiyo
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akipata picha ya pamoja na waandaaji wa semina hiyo pamoja na wadau wengine kutoka Serikalini. Semina hiyo imefanyika mapema leo Machi 30.2016, jijini Dar es Salaam.