Monday, August 6, 2012

SAMATTA ‘NOUMA’ TP MAZEMBE



MSHABULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta anayekipiga katika klabu ya TP Mazembe ya DR Congo, amezidi kuonekana mkombozi kwa timu hiyo baada ya kuifungia bao la ushindi katika mchezo wao dhidi ya Zamalek ya Misri, kwenye michuano ya Klabu bingwa Afrika.

Samatta ambaye alipiga msumari wa mwisho katika ushindi wa mabao 2-0, alipata bao hilo dakika ya 77 huku la bao kwanza lilifungwa na Isaac Kasongo wa Zambia, katika dakika ya 70, katika mechi ilyochezwa mjini Lubumbashi.

Mazembe, kwa sasa imeshika nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi B na kuipiku Bachem Chelsea ya Ghana, iliyokubali kichapo cha mabao 4-1 kutoka kwa vinara wa kundi hilo Al Ahly ya Misri wanaoongoza kwa pointi 9.

Mechi za kundi A, zilitarajia kuendelea jana ambapo vinara wa kundi hilo Esperance ya Tunisia, walikuwa wenyeji wa ES Sahel, huku Sunshine Star ilikuwa nyumbani kuwakaribisha ASO Chlef.

Timu mbili za juu katika msimamo kwa kila kundi zitafuzu hatua ya nusu fainali.
Chanzo: Mtanzania

No comments:

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa