▼
Tuesday, August 7, 2012
NI WAZO TU !!!!
ILI KUPUNGUZA MATUMIZI TUFUATE HAYA KWA MAKINI
KUTOKANA NAMATATIZO YA KIUCHUMI YALIYOKO TAFADHALI WAFANYAKAZI WOTE WA SERIKALI YANGU WATALAZIMIKA KUFUATA TARATIBU HIZI ILI KUPUNGUZA MATUMIZI
Malazi:
Watumishi wa ngazi za Uwaziri mnashauriwa kulala kwa ndugu zenu na marafiki wakati mkiwa katika ziara za kikazi. Wafanya kazi wa ngazi za chini ya hapo tumieni madarasa, vituo vya basi au hata vibaraza vya ofisi mtakazozitembelea kwa ajili ya kujihifadhi wakati wa usiku.
Usafiri:
Ni busara kubwa kuomba lifti kila uwapo katika shughuli za kazi. Waheshimiwa Mawaziri na hata wabunge watumie mabasi na hatimae treni mara zitakapoanza kufanya kazi. Usafiri wa ndege utatolewa pale ambapo ni lazima kwa mfano ikiwa utalazimika kufanya kazi wakati unaumwa au wewe ni Rais.
Chakula:
Ulafi ni hasara, hindi la kuchoma na maji vinaweza kabisa vikakufikisha siku ya pili. Kwa viongozi ndizi sukari mbili tatu za ziada zinashauriwa.
IT CAN BE DONE PLAY YOUR PART
chanzo: http://chekanakitime.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa