Friday, April 27, 2012

Breaking News: Jk Avunja Baraza la Mwaziri


Katibu NEC,Itikadi na Uenezi CCM Ndg. Nape Nnauye
Baada ya Kamati kuu ya chama tawala CCM kukutana leo jijini Dar Es salaam chini ya Mwenyekiti wao Dr. Jakaya Mrisho Kikwete,imeridhia kulivunja baraza la mawaziri wa serikali ya Jamhuri ya Muungano baada ya baadhi ya mawaziri na watendaji wa umma pamoja na mashirika ya umma kuhusishwa na ubadhirifu wa fedha za umma.
 Akiongea jijini Dar es salaam baada ya mkutano huo, Katibu NEC,Itikadi na Uenezi CCM Ndg. Nape Nnauye amesema kwamba Kamati imewapongeza kamati teule ya baraza la wawakilishi Zanzibar kwa ripoti yao, na pia kuwapongeza wabunge kwa kujadili wazi ripoti ya Za Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali ambapo ndio mapungufu hayo yaliibuliwa.
 Nnauye amesema kwamba Rais Jakaya Kikwete ameamua kulisuka upya baraza lake la mawaziri na kuahidi kuwajibisha wale wote waliokutwa na hatia za ubadhirifu wa fedha za umma.

Ingawa hofu ilitanda nchini kana kwamba baraza la mawaziri lisingevunjwa na watendaji hao kutowajibishwa kama baadhi ya vyombo vilivyoandika,Tunampongeza Rais Kikwete kwa uamuzi huu muhimu na nyeti kwa kusuluhu taifa.

Mungu ibariki Tanzania

No comments:

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa