Thursday, March 15, 2012

UJUMBE WA LEO !!!!!!

Dar es Salaam, Februari 9, 2012: Watu wenye wapenzi wengi wapo katika hatari zaidi ya kuambikizwa Virusi vya UKIMWIHIV ukilinganisha na wale wenye mpenzi mmoja, shirika la PSI/Tanzania limesema.
Tabia hii ambayo imeelezwa kuwa ni maarufu miongoni mwa vijana wa Kitanzania imeelezwa kuwa ndiyo chanzo kikubwa cha kuenea kwa maambukizi ya UKIMWI nchini. Hali ya maambukizi ya UKIMWI nchini kwa sasa ni asilimia 5.7 kwa mujibu wa utafiti wa kitaifa wa mwaka 2008.
 "Ni muhimu sana hasa kwa vijana, ambao ni nguvu kazi ya taifa kupunguza na kuacha kabisa tabia ya kuwa na wapenzi wengi na kuhakikisha kuwa mara zote wanatumia mipira ya kondom wakati wa tendo la kujamiiana,” alisema Dk Alex Ngaiza Mtaalamu Mshauri wa program ya UKIMWI ya PSI/Tanzania.
Akionesha msisitizo mkubwa katika tabia ya kuwa na wapenzi wengi na kusisitiza kuwa ni kichocheo kikubwa katika maambukizi ya virusi vya UKIMWI Dk Ngaiza alisema: "Kuna fikra au tuseme tabia ya baadhi ya watu kufikiria kuwa kwa kuwa na wapenzi wengi kunaweza kutatua baadhi ya matatizo yao ya kiuchumi au kijamii lakini ukweli ni kuwa kwa kadri unavyokuwa na wapenzi wengi ndivyo hivyo nafasi yako ya kupata maambukizi inavyokuwa kubwa,” alisisitiza.
Kwa kuzingatia jinsi tatizo hilo lilivyo kubwa hapa nchini ambapo kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2008 kwa wanandoa au wapenzi wanaoishi pamoja, asilimia 25 ya wananchini walikiri kujihusisha na mapenzi ya zaidi ya mpenzi mmoja. Dk Ngaiza akasema kwa kuzingatia hilo PSI/Tanzania inatarajia kuanzisha kampeni maalumu kuelimisha wananchi juu ya madhara ya kujiingiza katika mtandao wa mapenzi.
Katika hafla hiyo fupi, PSI ilitoa jumla ya katoni 45 za Salama kondom kwa washiriki wa Shindano la Bongo Star Search wa mwaka jana ambao walishinda katika zoezi la kuuza bidhaa hizo zaidi ya pakiti 40 ndani ya dakika tano. Washindi waliokabidhiwa zawadi zao ni mshindi wa kwanza wa mashindano hayo kwa mwaka jana, Haji Ramadhani aliyekabidhiwa katoni (20), Waziri Salum (10), Rogers Lucas (10) na Bela Kombo (5).
Kuhusu PSI/Tanzania
PSI/Tanzania ni shirika lisilo la kiserikali linalotoa elimu na huduma za afya katika maeneo ya UKIMWI, Malaria, Magonjwa ya kuharisha na Afya ya Uzazi. Likifanya kazi kwa kushirikiana na sekta binafsi na serikali, PSI/Tanzania inatumia mbinu na njia za masoko. Shirika linatoa bidhaa za kuokoa maisha, huduma za kliniki na elimu ya kubadili tabia ambazo zote zinalenga katika kuwawezesha Watanzania wahitaji kuishi wakiwa na afya nzuri.

Tofuti: www.psi.or.tz Twitter: twitter.com@PSIHealthyLives Face Book: PSI/Tanzania

No comments:

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa