Saturday, October 22, 2011

Nakaaya aachana na siasa



Nakaaya Sumari


HERIETH MAKWETTA
MSANII wa muziki wa kizazi kipya ambaye pia aliwahi

 kujihusisha na masuala ya siasa nchini, Nakaaya Sumari,
 amejutia uamuzi wake wa kugeukia siasa, akisema amepoteza 
muda mwingi pasipo manufaa yoyote.

Nakaaya ambaye aliwahi kushiriki katika mashindano ya kwanza

 ya Tusker Project Fame mwaka 2006, sasa ameamua kuachana
 na siasa kwa lengo la kuutumia muda wake kuelimisha jamii 
kupitia muziki.

�Nimegundua nilifanya maamuzi yasiyo sahihi, katika kipindi 

chote nilichokaa ndani ya siasa haijanisaidii chochote hivyo
 nimeamua kujiondoa. Nitabaki kwenye muziki tu ambako ndiko
 kipaji changu kilipo,� alisema Nakaaya.

Msanii huyo aliyewahi kutamba na wimbo wa Mr Politician,

 alijiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
 mwaka 2009 na baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, 
alihama na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).

No comments:

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa