Saturday, September 3, 2011

eti Baba Riz Awatosa Waislamu, Na Mahaskofu Wamshabikia????



Baba Riz aliwageuka waislamu alipoutubia Baraza la Idd katika Msikiti wa “Gaddafi” mjini Dodoma  juzi, Kinyume na ahadi zake alizotoa yeye na Chama Cha Magamba wakati wa uchaguzi wa mwaka 2005/2010, kuhusu serikali kusaidia kuanzishwa Mahakama ya Kadhi.

Pamoja na mambo mengine Baba Riz alisema Wakristo nchini hawahusiki na kuchelewa kwa mchakato wa kuanzishwa kwa mahakama ya kadhi.
“Nilipokutana na Jukwaa la Maaskofu Julai 22, mwaka huu walisema ngoja ninukuu…… Kuanzisha Mahakama ya Kadhi nchini ni  jambo zuri linalowahusu Waislamu. Kwa kuwa ni jambo la kidini waachiwe Waislamu wenyewe walifanye ndani ya Uislamu, pasipo kutumia hazina ya Serikali ambayo ni fedha ya walipa kodi wote nchini…,”
Kwa nyakati tofauti wakizungumzia hotuba hiyo baadhi ya maaskofu akiwemo Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Yuda Thedeus Ruwai’chi, alimpongeza mkuu huyo wa nchi kwa hotuba hiyo nzito.
Ruwai’chi ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Mwanza alisema: “Kauli kama za jana zingekuwa zinatolewa mara kwa mara,  masuala mengi ya nchi yangeshapata ufumbuzi, nimesoma hotuba hiyo kwenye magazeti, lakini nitafurahi sana nitakapopata hotuba yenyewe niisome kwa mtiririko wake”.
Kuhusu suala la Mahakama ya Kadhi, Askofu Ruwai’chi aliunga mkono kauli ya Rais Kikwete kuhusu waumini hao kuanzisha mahakama hiyo wenyewe na kusisitiza kuwa Waislamu ni watu wazima wasiotaka kubebwa na mtu yeyote ili kufanikisha mambo yao.
Askofu Ruwai’ch alifafanua: “Wakianzisha wenyewe Mahakama ya Kadhi hakuna anayewazuia…, kwa sababu ni dini isiyohitaji kubebwa, waanzishe chombo chao kisicho cha Serikali, wakiendeshe kwa fedha zao wenyewe”.
Hata hivyo, alisema, bado Serikali inaonekana kuwa na kigugumizi juu ya suala la mahakama hiyo, ndiyo maana kuna kauli zinazogongana.
Rais huyo wa Tec badala yake alisema, “Mara anasema suala lipo kwa Waziri Mkuu, mara waanzishe wenyewe…, wasijing’ate, wawaambie tu kuwa waanzishe mahakama yao kwa fedha zao na waiendeshe wenyewe”.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Askofu Peter Kitula, alisema hotuba ya Rais Kikwete ni nzuri na imeweza kutoa ufafanuzi wa mambo mengi yaliyokuwa yakiikabili nchi.
Askofu Kitula ambaye pia ni Askofu wa Kanisa la African Inland (AICT),Dayosisi ya Mara na Ukerewe alifafanua: “Hotuba ni nzuri, haikuegemea popote…, imetoa ufafanuzi kwa mambo mengi ya nchi na msimamo wa Serikali tumeuona”.
Kuhusu suala la Mahakama ya Kadhi, naye alisisitiza kwamba, inatakiwa ianzishwe na Waislamu wenyewe na uendeshwaji wake pia ufanywe na dini husika na isiwe na kufanya ujanja wa kuianzisha na baadaye Serikali ikajiingiza katika kuiendesha.

No comments:

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa